Mwanamuziki wa zamani ambaye kwa sasa ni mwanasheria, Esther Wassira
amewatupia shutuma nzito madaktari wa hospitali ya Amana ya jijini Dar
es Salaam kwa kile alichokiita ‘uzembe’ wa makusudi uliosababisha kifo
cha mtoto mchanga wa rafiki yake.
“Naenda pia kwenye msiba wa rafiki yangu amefiwa na mtoto wake wa siku
moja,aliyefia hospitali Amana,baada ya Madaktari kuwachomolea watoto
ishirini Oxygen na kuwaacha wakiteketea!!! Kweli jamani??? Doctors???
You can kill innocent infants??? Si mngewaachia hiyo oxygen tu
mkaondoka??? Serikali!!! Do something jamani..! Just give them what they
want!! Think of the loss..mama abebe mimba miezi tisa,mwanae auliwe?”
Esther aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“This is a catastrophe to the nation..hivi kweli!!!!, it is very
serious..yupo kwa mama yake anakandwa tumbo na mwanae ameshamzika!!!
This is BAD! Naogopa nchi yangu!!”
Hata hivyo shutuma hizo nzito dhidi ya madaktari wa Amana zilizotolewa
na mwanadada huyo zilipokelewa kwa hisia tofauti kutoka kwa watu
wengine.
“Pole na msiba huo..ila usiwe unakurupuka na kuleta uzushi kuwa
madaktari wamewachomolea oxygen watoto..ukiambiwa thibitisha sijui
utasemaje…u r a lawyer..think before u leap….usiwe kama layperson
kukurupuka na kusema habari za uvumi….madaktari sio wajinga kama
serikali yako kufanya kitu kama hicho kwa infants kama hao….kifo cha
watoto ni kawaida tu..kama ingekuwa hakuna huu mgomo na kukatokea hilo
sidhani kama ungesema hivyo Esther,” aliandika mtu mmoja aitwaye Pedro
Juan.
“Pedro usinifrustrate!! I have enough frustrations!!! Ninakwambia am
sitting with a woman hapa my friend ananiambia exactly what has happened
wewe unaniambia uzushi!!! Ni heri ushtuke na uombe kuliko kunistress
zaidi..do you think I want to accuse doctors au unadhani nafurahi kuona
insensitivity ya government!! Am a human being,a woman for that matter!!
Lawyer or not!!!,” alijibu Esther.
Mtu mwingine aitwaye Isaac Ruge Abraham alisema, “Nimeisoma hii post na
kusikitika sana.Mimi na daktari kwa miaka 6 sasa na siamini kabisa kama
kuna daktari anaweza kuchomolea watoto oxygen kwa madai yake.Kama
amefanya hivyo ni kosa la jinai.Ila kama kuna mgomo na daktari hakwenda
wodini kwa sababu kuna mgomo haya ni mambo mawili tofauti.
Kwa sasa mgomo umekamata pabaya maana hakuna hata emergencies
zinazoguswa na ni kipindi kibaya sana kuumwa hata kama wewe ni
daktari.Nadhani ni vibaya kutumia maelezo ya upande mmoja na kuyatumia
kuweka presumptive judgement.
Esther Wasira mdogo wangu.Kwa kazi hii madaktari hujitoa mara zote
wanapofanya kazi wakati mwingine bila kulala hadi masaa 36 na sidhani
mtu anayejitoa kiasi hicho anaweza kufanya jambo kama ulilolielezea
hapo.Wapo wazembe kwenye hii fani lakini hakuna wa kutenda hivi na kama
yupo basi hafai kufanya fani hii.”
Kwa upande wake Esther aliongeza kwa kusema, “Isaac I do understand you
brother..na wewe kama daktari umejibu vyema tena very objectively!! As
you say,ni ngumu kuamini kuna daktari angekuwa mnyama kiasi hiki..what
this lady was narrating on the incident ya mwanae,anasema,it was
chaotic, they were many of them,charged into the room and switched them
off,as a sign of “no more service guys”..!
Mimi nili-panic sana asubuhi..huyu mtu msibani anasema “cause of death”
ni mwanangu kutolewa oxygen wakati akiwa Amana anaendelea na matibabu!!
So as u say,it might be a presumptive judgment based on the testimony of
the mother,but am not pronouncing anybody guilty!! I said earlier,if it
gets to the level where the issue has been taken to the hands of the
law and the accused tried,the state will declare their status,whether
innocent or guilty!! Take this as a charge sheet,that’s the
accusation,kinywa cha Mtanzania aliyepoteza mtoto wake ndio kimenena
hayo!! So treat me as a spokesperson right now!!”
Mgomo wa madaktari nchini unaendelea kuchukua sura mpya kila
kukicha,ambapo juzi Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari nchini Dr.
Stephen Ulimboka, alitekwa na watu wasiojulikana walimpiga kinyama. Kwa
sasa bado amelazwa katika hospitali ya Muhimbili akiendelea kupewa
matibabu.
No comments:
Post a Comment