Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye kulia akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za TFF, mchana huu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah. |
Na Prince Akbar
MABINGWA
watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame
watafungua dimba na Atletico ya Burundi katika mchezo wa Kundi C wa
michuano hiyo, Julai 14, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliowekwa Kundi A, wataanza na
URA ya Uganda Julai 16, kwenye Uwanja huo huo.
Wawakilishi
wengine wa Tanzania katika michuano hiyo, Azam FC wao wataanza na
Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa Chamazi, Julai
15.
Katibu
Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA),
Nicholaus Musonye amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari mchana
huu, ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam
kwamba, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) itashiriki
kama timu mualikwa.
Aidha,
habari za kusikitisha ni kwamba, Musonye amesema Sudan, Ethiopia,
Eritrea na Somalia hazitaleta wawakilishi wao kwa sababu mbalimbali.
Wakati
Ethiopia ligi yao inaanza wiki hii, Sudan wawakilishi wao wapo kwenye
michuano ya Afrika na wameshindwa kuteua timu mbadala, Somalia
wawakilishi wao Elman wamebadilisha uongozi, hivyo bado hawajajipanga na
Eritrea kutokana na desturi ya wachezaji wao kuzamia kila wanapokuja
kwenye mashindano, wameondolewa.
“Wameondolewa,
kwa sababu mbili, kwanza nchi yao imeomba ipewe muda kulifanyia kazi
sual hilo, na sisi pia (CECAFA) tunalitafutia ufumbuzi,”alisema Musonye.
Lakini
Musonye amekiri kitendo cha kuyatoa mashindano hayo mwanzoni mwa mwaka
hadi katikati ya mwaka kumechangia baadhi ya timu kutoshiriki na amesema
tayari amewasilisha pendekezo kwenye Mkutano Mkuu, mashindano yarejee
kufanyika mwanzoni mwa mwaka kama ilivyokuwa awali.
Kuhusu
mechi ya ufunguzi ya Simba kuchezwa Julai 16, ambayo itakuwa Jumatatu
badala ya Jumapili, Musonye alisema kwamba imetokana na kwamba Julai 15,
Uwanja wa Taifa kutakuwa na fainali za Copa Coca Cola, ambayo
maandalizi yake yote yamekamilika.
Yanga ndiye bingwa mtetezi wa mashindano, baada ya kuifunga Simba SC katika fainali mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
RATIBA KAMILI KOMBE LA KAGAME
No comments:
Post a Comment