Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, June 13, 2012

Lita elfu tisa za gongo zakamatwa Namanga mkoani Arusha


Na Gladness Mushi wa Fullshangwe
JESHI la polisi mkoani Arusha limefanikiwa kukamata lita elfu tisa za pombe haramu aina ya Gongo ambayo ilikuwa inatokea nchini Kenya na kuingizwa Tanzania kwa njia za Magendo
Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Bw Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 10 majira ya saaa kumi na mbili za jioni katika eneo la Namanga
Alisema kuwa kufanikiwa kukamatwa kwa pombe hiyo haramu aina ya Gongo kunatokana na Taarifa kutoka kwa raia wema ambapo ndio waliotoa taarifa kwa jeshi hilo na jeshi hilo likaanza  msako maalumu
Kamanda huyo alisema kuwa mara baada ya taarifa hizo askari walirfanya doria ndani ya eneo hilo la Namanga  na walifanikiwa kumkamata raia mmoja wa kitanzania ambaye alijulikana kwa jina Nicoulaus Thobias(35) akiwa katika katika eneo hilo lita hizo za gongo ambazo zililkuwa kwenye mapipa 150
Aliendelea kusema kuwa mara baada ya kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo askari waliamua kufanya upekuzi katika gari lake na kumkumta na pombe hiyo haramu ambayo aliitoa nchini Kenya na kuileta Tanzania kwa ajili ya matumizi ambayo bado hajafahamika
“hapa mara baada ya kukamtwa askari hao walikagua gari alilokuwa nalo  mtuhumiwa huyo ambalo ni Scania  lenye namba za usajili  T 416 AJX ambalo linamilikiwa na Joseph Masawe ambapo mara baada ya hapo mtuhumiwa aliwekwa chini ya ulinzi’aliongeza kamanda Sabas
Pia alisema kuwa mtuhumiwa huyo alipohojiwa juu ya pombe hiyo haramu alidai kuwa pombe hiyo si pombe bali ni Spirit jambo ambalo halikuwa kweli na badala yake alikuwa anadanganya Polisi
Hata hivyo Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika ambapo pia gari nalo bado linashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi

No comments:

Post a Comment