Na Blog ya Francis Godwin
katibu
wa itikadi na uenezi wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Taifa Bw. Nape Nauye
amekiri kuwa CCM ilipoteza jimbo la Iringa mjini kwa makosa yake na
kuwa kosa hilo kamwe halitarudiwa tena na kumfananisha mbunge wa jimbo
hilo Mchungaji Peter Msigwa kuwa ni msindikizaji wa CCM katika jimbo
hilo.
Kwani alisema kuwa kosa lililofanyika
katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 kwa kushindwa kuongoza kura za ubunge ni
kutokana na makosa yaliyojitokeza hivyo kupelekea madiwani kushinda na
Rais Jakaya Kikwete kupata ushindi mkubwa ila ubunge baada ya yule
waliomchagua wana CCM Frederick Mwakalebela jimbo hilo lilichukuliwa na
upinzani kosa ambalo kamwe halitarudiwa tena.
Asema
vyama vya upinzani ni vyama vya wanaharakati kwa ajili ya kuikumbusha
serikali ya CCM kwa pale inapokosea na sio kuja kuongoza nchi.
Pia
Nauye aliuagiza uongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa kuhakikisha
unafungua mara moja barabara ya Magereza inayoelekea Hospitali ya mkoa
ambayo imekuwa ikichangia usumbufu wa wagonjwa Kwenda kutibiwa.
Akiwahutubia
wakazi wa jimbo la Iringa mjini katika viwanja vya Soko kuu Leo ,Nauye
alisema kuwa moja Kati ya kilio kikubwa kwa wakazi wa mji wa Iringa ni
hatua ya uongozi wa Magereza Iringa kuifunga barabara hiyo kwa ajili ya
matumizi ya Magereza mkoa wa Iringa jambo ambalo linasababisha usumbufu
kwa wananchi wanaofika Hospitali hiyo ya mkoa.
Hivyo
alisema tayari amemwagiza mkuu wa mkoa wa Iringa DKT Christina
Ishengoma kuhakikisha anasimamia zoezi hilo ili barabara hiyo ifunguliwe
na kupunguza kero za wananchi na wagonjwa wanaofika kutibiwa katika
Hospitali hiyo ya mkoa.
No comments:
Post a Comment