Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
akikagua shamba la nyanya na mazao mengine ya mboga pamoja na mizabibu
katika shamba linalomilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade,
lililopo kijiji cha Chikopelo,wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma leo
asubuhi. Kushoto ni mmoja wa wamiliki wa Shamba hilo Bwana Alon Hoven,
anayeshirikiana na Bwana Dunstan Mrutu (hayupo pichani). Shamba hilo
linamwagiliwa kwa kutumia teknolojia ya matone (Drip irrigation
system).
Mmoja wa Wamiliki wa Shamba la Mboga
katika kijiji cha Chikopelo Bwana Alon Hoven, kimwonesha Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, baadhi ya mazao yanayozalishwa kwa kutumia
mbegu bora pamoja na teknolojia ya ya umwagiliaji wa matone wakati Rais
alipotembelea shamba hilo katika kijiji cha Chikopelo, wilayani
Bahi,mkoani Dodoma leo asubuhi.Shamba hilo lenye ukubwa wa hekari mia
moja linamilikiwa na kampuni ya kilimo ya Tendaji Trade, chini ya Bwana
Dunstan Mrutu na Alon Hoven raia wa Israel.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo,
Rais Kikwete alisifu juhudi za wawekezaji hao kwa kutumia mbinu za
kisasa za kilimo na kuwaasa wanakijiji wa Chikopelo kujifunza mbinu bora
za kilimo hicho cha mboga ili waweze kupata ufanisi na kuboresha maisha
yao. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaonya viongozi wa kijiji cha
Chikopelo kutoendelea kuuza ardhi yote kwa wawekezaji na badala yake
kutunza na kuilinda kwaajili ya kizazi kijacho.
No comments:
Post a Comment