Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Joseline Kamuhanda,kiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kampuni ya Vodacom Tanzania kuwa mdhamini mkuu wa Mawasiliano na matangazo wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba)yatakayoanza hivi karibu jijini Dares salaam,Vodacom Tanzania ndiyo wadhamini wakuu wa Mawasiliano kwa vyombo vya habari katika kipindi chote cha Maonyesho hayo,Kulia Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara Tanzania(Tan Trade)Bw.Samwel Mvingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara Tanzania(Tan Trade)Bw.Samwel Mvingira(kulia)akipokea modem pamoja na simu ya mkononi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Joseline Kamuhanda,kwa ajili ya Mawasiliano wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (sabasaba)yatakayoanza hivi karibu jijini Dares salaam,Vodacom Tanzania ndiyo wadhamini wakuu wa Mawasiliano na matangazo kwa vyombo vya habari katika kipindi chote cha Maonyesho hayo.
Baadhi ya waandishi wa habari na
maofisa wa Vodacom Tanzania wakifatilia mkutano wa Vodacom Tanzania
kujitangaza rasmi kuwa wadhamini wakuu wa Mawasiliano na matangazo kwa
vyombo vya habari katika kipindi chote cha Maonyesho ya Biashara ya
Kimataifa (sabasaba)yatakayoanza hivi karibu jijini Dares salaam.
Kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom
Tanzania leo imeingia katika ubia na Mamlaka ya Maendeleo na Biashata
Tanzania (TanTrade) kama mdhamini maalum katika sekta ya mawasiliano
kwenye maonyesho ya Kimataifa ya biashara Dar es Salaam.
Vodacom Tanzania itaendesha matangazo
na vyombo vya habari kabla na baada ya maonyesho ndani ya siku kumi za
maonyesho hayo ya kibiashara ambayo yataanza tarehe 30 ya mwezi juni.
Ushirikiano huu umekuja wakati ambapo
sekta ya mawasiliano imekuwa na changamoto tangu mfumo wa kimaisha ya
Kijamaa. Ambapo watanzania wanatumia huduma ya simu kama njia ya
kubadilishana mawazo katika ngazi ya familia na shuguli za kiofisi.
Vodacom Tanzania imeingia katika
ushirikiano huu huku imafanikio yake katika sekta ya mawasiliano ndani
ya nchini Tanzania. Kampuni imekuwa ikitambulika kwa kupiga hatua zaidi
katika kuhakikisha kuwa wateja wanatumia simu sio tu katika mawasiliano
bali hata katika huduma za kifedha.
"Tumegundua hili na ndio maana tukaleta
huduma ya kuamisha fedha ya Vodacom M- PESA, hivi sasa huduma hii
imekuwa ni ya msingi kwa Watanzania walio wengi kutokana na huduma
mbalimbali wanazopata kama kufanya malipo mbalimbali na kuhamisha fedha
kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine" alibainisha Mkurugenzi mtendaji wa
Vodacom Tanzania Rene Meza.
Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa
Vodacom Tanzania inajitahidi kutoa huduma na bidhaa ambazo ni rahisi na
nafuu kwa wateja wote nchini.Katika maboresho ya hivi karibuni, Vodacom
Tanzania imezindua huduma mbalimbali ambazo ni maalum kwa vijana ikiwemo
kampeni ya wajanja na Wajanja internet, huduma ambazo zinatoa nafasi
kwa vijana kupata huduma na bidhaa nafuu kutoka Vodacom alisema Rene.
Vodacom Tanzania imewekeza kwa kiasi
kikubwa katika maendeleo na maboresho ya miundombinu, kupitia hili
kampuni inatarajia kuboresha ubora wa huduma na bidhaa zinazotolewa kwa
wateja, ambapo sasa wataweza kumudu gharama za huduma na bidhaa hasa kwa
vijana ili kuongeza watumiaji wa huduma na hadhi ya Kampuni..
Maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam
Maarufu kama sabasaba, Ni maonesho ya kibiashara yanayoongoza Tanzania
Maonyesho hayo yanayofanyika kwa siku kumi huvutia wageni zaidi ya
350000 na kujenga mahusiano na maingiliano baina ya watoa huduma na
wateja wao na kutoa fursa kwa wateja kuangalia na kulinganisha ubora wa
bidhaa. Kutoka Haki Ngowi: www.hakingowi.com
No comments:
Post a Comment