
Ushindi wa Czech umewaondoa wenyeji PolandPetr
Jiracek alifunga bao la pekee katika mechi ya uwanja wa Wroclaw dhidi
ya wenyeji Poland siku ya Jumamosi, na kuwahuzunisha mashabiki wa
nyumbani, wakati Jamhuri ya Czech ilipofuzu kuingia robo fainali za
mashindano ya Euro 2012.
Jamhuri ya Czech imefuzu katika kundi hilo, baada ya kuongoza kwa pointi 6.
Jiracek, kiungo cha kati wa timu ya
Wolfsburg ya Ujerumani, aliweza kuutambariza mpira wavuni katika sehemu
ambayo kipa Przemyslaw Tyton hakuweza kuwa na matumaini kabisa ya
kuufikia mpira, zikiwa zimesalia dakika 18 tu mechi hiyo kumalizika.
Poland walianza mechi wakifahamu
kwamba iwapo wangelipata ushindi katika mechi hiyo, basi wangeliweza,
kwa mara ya kuwanza, kuwa miongoni mwa timu nane ambazo zingelisalia
katika mashindano kushiriki katika mechi za robo fainali.
Nahodha wa Poland Jakub
Blaszczykowski, katika juhudi za dakika ya mwisho alikuwa nusra afunga
bao la kusawazisha, lakini ulinzi wa Czech ulikuwa thabiti, na mpira
kuondolewa kabla ya kuvuka msitari.
No comments:
Post a Comment