Mfanyabiashara wa nyama mjini Iringa Sijali Nyomolelo akipelekwa wodini asubuhi hii
eneo la ajali watu wakiwa wamejaa kushuhudia
hivi ndivyo ilivyokuwa katika ajali hiyo
Mfanyabiashara
wa duka la nyama (bucha) katika eneo la Mwembetogwa mjini Iringa
Bw Sijali Nyomolelo amepata ajali mbaya ya gari asubuhi ya leo eneo
la Ikonongo katika Manispaa ya Iringa.
Katika ajali hiyo mfanyabiashara huyo ambaye alikuwa na gari ndogo Taxi yenye namba za usajili T 150 AAM akielekea maeneo ya barabaera ya Pawaga- Iringa ,alikuwa peke yake katika gari hiyo .
Mashuhuda wa ajali hiyo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa kabla ya ajali hiyo kutokea mfanyabiashara huyo alionekana akiendesha gari hiyo kwa mwendo mkali mfano wa gari ya mashindano hivyo kupelekea gari hiyo kumshinda na kuhama barabara kabala ya kugonga mti uliokuwa upande wa kushoto mwa barabara hiyo.
Walisema kuwa baada ya ajali hiyo jitihada mbali mbali za wasamaria wema zilifanyika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kulivuta gari hilo kwa kamba ili kumtoa mfanyabiashara huyo ambaye alikuwa amenasa katika gari hilo.
Pamoja na jitihada hizo bado vikaba waliweza kulizunguka gari hilo na wakati wengine wakiokoa baadhi waliweza kumsaji na kumpora kila kitu alichokuwa nacho zikiwemo fedha ,simu na vitu mbali mbali.
Baadhi ya rafiki wa karibu na mfanyabiashara huyo wanadai kuwa mfanyabiashara huyo ambaye awali alikuwa na usafiri wa piki piki alipata kupata ajali siku za nyuma na kuvunjika mguu na baada ya kununua gari hilo bado aliendelea na mwendo mkali kama wakati akimiliki piki piki na walipojaribu kumuonya juu ya mwendo kasi ndipo alipoandika nyumba ya kioo cha Taxi hiyo kuwa MAISHA NI KUTAFUTA SIO KUTAFUTANA
Akiongea kwa shida katika hospital ya mkoa wa Iringa mfanyabiashara huyo ambaye amevunjika mikono na miguu alisema kuwa katika gari hilo alikuwa na fedha nyingi japo hakutaja ni kiasi gani.
Habari na picha kwa Hisani ya Fransic Godwin Blog

No comments:
Post a Comment