Alumni wa Mlimani Primary wakishusha vitendea kazi.
Shule ya Msingi Mlimani ni moja kati
ya shule kongwe hapa Tanzania. Shule hii ilianzishwa miaka ya sitini na
hadi sasa imetoa vijana wengi wanaolitumikia Taifa la Tanzania kwenye
Nyanja mbalimbali. Shule hii iliyopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es
salaam. Vijana wengi wa Chuo Kikuu, Savei, Makongo, Sinza, Kimara na
maeneo ya karibu wamepita hapo Kutokana na kula chumvi nyingi, majengo
na miundo mbinu ya shule hii iamechoka. Ili kuboresha majengo vijana
waliosoma hapo wakajikusanya na kuanzisha ‘’ Giving Back to Mlimani
Day’’. Mwaka huu siku hii iliangukia jumamosi ya Tarehe 30 June 2010.
Alumni wa Mlimani wanawashukuru mno wadau waliotoa; Jasho, Fedha , Muda
na kusaidia kufanikisha shughuli hii.
No comments:
Post a Comment