Mwananchi wa kijiji cha Mzuri
Makunduchi Bakari Ubwa, akitoa maoni yake mbele ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, ametaka kuwe na Serekali mbili ya Zanzibar na Tanzania Bara na
kila Serekali iwe na uwezo wake na Rais wa Zanzibar awe na uwezo wa
kuamua mambo yake kwa ajili ya Zanzibar,Rais wa Zanzibar awe na uwezo wa
kuchagua Mabalozi kwa ajili ya Zanzibar na Rais wa Tanzania pia na yeye
achaguwe mabalozi wa Tanzania.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Balozi Salim Ahmed Salim, akizungumza kuhusiana na utoaji wa
maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania katika mkutano huo uliofanyika
viwanja vya Mtende.
Mwenyekiti wa Mkutano wa kutowa
maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania Mohammed Yussuf Mshamba,
akisoma vipengele wakati wa kutowa maoni ya mabadiliko ya katiba katika
viwanja vya Mtende Makunduchi.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Tanzania Dk Mvungi, akitowa maelezo kwa Wananchi wa Kijiji cha
Mtende waliofika kutoa maoni yao katika viwanja vya Skuli ya Mtende.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Tanzania wakifuatilia maoni ya Wananchi wa Kijiji cha Mzuri
wakiyatowa mbele ya Tume hiyo ilioanza kazi yake jana katika Wilaya ya
Kusini Unguja Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Mwananchi wa Kijiji cha Mzuri
Makunduchi akikabidhi barua yenye maoni yake kuhusu Mabadiliko ya
Katiba, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya mpira timu ya Mwenge
Mzuri,
Mwananchi wa Kijiji cha Mtende
Makunduchi Aziza Mcha, akikabidhi barua yake yenye maoni yake kwa
Mwenyekiti wa Mkutano wa kutowa maoni ya mabadiliko ya Katiba ya
Tanzania Mohammed Yussuf Mshamba, wakati tume hiyo ilipofika katika
Wilaya ya Kusini Unguja kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Katiba,
mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Skuli ya Mtende.
Mwananchi wa Kijiji cha Mtende Ali
Khamis Ali, akichangia maoni yake kwa kuanza kwa historia kuhusu Mzee
Karume, ambaye amesema Unguja itakuwa kama peponi na kweli ilikuwa hivyo
kwa kujenga Nyumba za Wazee Sebleni na kuanzisha Viwanda mbalimbali
katika Zanzibar.Amesema kuwepo kwa serikali mbili ya Zanzibar na
Tanganyika na kutaka kuwe na Muungano wa Mkataba na kugawana sawa kwa
sawa misaada inayopatikana. na mambo ya muungano kugaiwa sawa.
Mwananchi wa Kijiji cha Mzuri
Makunduchi Duli Ali Duli, akichangia maoni yake kwa Tume iliofika
kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania,
amesema kuwe na Serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika, na kuondoa
kasoro zilioko katika Muungano huu.
Mwananchi wa Mtende Abuu Kombo
Ramadhani, ametowa maoni yake kuwe na serekali mbili na kuwe na uwiano
katika nafasi za Muungano kwa pande mbili hizi na Zanzibar iwe na
rasilimali zake wenyewe bila kuingiliwa na upande mwengine. na bara iwe
hivyohivyo.
Mwanaichi wa Kijiji cha Mtende Mohammed
Shaka Mussa, amesema nashukuru kuitwa Tanzania na pia Umoja ni
Nguvu,Utengano ni Udhaifu. Amesema kuwepo na serikali mbili ya Zanzibar
na Tanganyika na kila upande uwe na uwezo wa kuamua mambo yake na
kuondoa kasoro za Muungano zilizopo ili kuimarisha umoja wetu.
Wananchi wa Kijiji cha Mzuri
Makunduchi wakiwa katika viwanja vya Mwenge wakishiriki kutowa maoni yao
wakisikiliza maoni ya Wananchi mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Tanzania.iliyofika katika kijiji hicho kukusanya maoni ya Wananchi.
Wananchi wa Kijiji cha Mtende
wakisikiliza maoni yanayotolewa na Wananchi wa Mtende mbele ya Tume ya
Marekebisho ya Katiba katika viwanja vya skuli ya Mtende
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Tanzania Balozi Salim Ahmed Salim. akibadilishana mawazo na Wazee
wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja, baada ya
kumalizika kwa utowaji wa maoni kwa Wananchi wa Kijiji hicho.Picha Zote
na Mdau Mapara Othman-Kusini Unguja
No comments:
Post a Comment