Mkurugenzi
wa Oparesheni wa Shirika la Ndega Tanzania (ATCL) Captain Richard Shaidi
(kulia) akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana juu ya
sababu zilizofanya ndege yao kushindwa kubeba abiria kutoka uwanja wa kimataifa
ya Kilimanjaro baada ya kupata ufa kwenye kiio cha mbele. Kushoto ni Mkurugenzi
wa Kiufundi Engineer Patric Itule. Picha na mwandishi wetu.
Na Mwandishi wetu
Ndege la Shirika la Ndege la
Tanzania (ATCL) jana lilipataufa kwenye kioo cha mbele kwenye chumba cha
Marubani na kushindwa kubeba abiria kwa sababu ya kiusalama.
Akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Oparesheni, Captain Richard Shaidi,
alisema ufa huo uliegundulika baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa, Kilimanjaro na kulazimika kukatisha safari yake ya kuelekea Mwanza
na kisha kurudi Dar Es Salaam.
Capt. Shaidi alisema ndege hiyo yenye
namba za usajili 4L AJB aina ya Boeing 737 – 500 isingebeba abiria kutokana na sababu
za kiufundi na kiusalama, ambapo ndege imerejea Dar Es Salaam bila abiria kwa
ajili ya matengenezo, kufuatana na kanuni za usalama wa Anga za kimataifa.
“Shirika linasikitishwa sana kwa
usumbufu uliojitokeza na uliotokea kwa abiria wake. Pamoja na tatizo hili,
Shirika limefanya utaratibu wa kuhakikisha kuwa abiria wanaendelea na safari
zao kwa kuwasafirisha kwa kutumia huduma ya ndege za mashirika mengine ya hapa
nchini,” alisema Capt. Shaidi.
Alisema matengenezo yanatarajiwa
kukamilika leo jioni na kuanza safari zake kama kawaida kesho nakuongeza kuwa wateja
wanaombwa kuwasiliana na ofisi zao au wakala wa shirika hilo.
SOURCE FULLSHANGWE
No comments:
Post a Comment