BODI
ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organization (MTTO), imelifuta
shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012, lililo fanyika New Mwanza
Hotel, juzi, huku taifa likiwa kwenye maombolezo ya siku tatu kutokana
na msiba mkubwa wa ajali ya meli ya Mv Skagit, mjini Zanzibar na
kupoteza uhai wa watu wengi.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari jana jijini Dar
es Salaam na kutiwa sahihi na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Miss
Utalii Tanzania, Abubakari Omary Bakari, ilisema shindano hilo
limefanyika kimakosa na matokeo yake hayawezi kutambuliwa kwa namna moja
ama nyingine.
Alisema
uamuzi wa serikali ni wa mwisho, hivyo hawajaunga mkono kufanyika kwa
shindano hilo wakati nchi ina majonzi ya kupoteza ndugu na jamaa wao.
“Shindano
limefanyika bila kuzingatia misingi ya kiubinadamu na uzalendo kwa
Taifa, hivyo Bodi imeamua kulifuta na waandaaji watafuata tena utaratibu
mwingine.
“Miss
Utalii ni shindano lenye uzalendo, hivyo inapotokea matatizo kama haya
na agizo la maaombolezo kutoka kwenye serikali nadhani kuna kila sababu
ya kuliafiki,” ilisema taarifa hiyo.
Shindano
hilo limeandaliwa na Fania Beauty Salon, chini ya Mkurugenzi wake Fania
Hassan, ambaye sasa ana changamoto nyingine ya kujiweka sawa katika
jamii, ukizingatia kwamba Taifa lilikuwa kwenye maombolezo
ya siku tatu.
No comments:
Post a Comment