eneo la tukio.
Ukumbi wa Sinema mjini Denver
Rais Barack Obama na mkewe Michele wameelezea masikitiko yao kufuatia mauawaji ya watu kumi na wanne mjini Denver huko Colorado.Obama alisema kuwa serikali itafanya kila juhudi kuwasaidia watu wa eneo la tukio, la Aurora wakati huu mgumu.Pia ameahidi kuwa serikali itakahakikisha aliyehusika anakamatwa.Mtu mmoja aliyekuwa amefunika uso wake kwa barakoa aliwauwa kwa kuwapiga risasi watu hao kumi na wanne na kuwajeruhi takriban hamsini wakati wa onyesho la filamu ya Batman, The Dark Knight Rises.Walioshuhudia tukio hilo kwenye kitongoji cha mji huo cha Aurora walisema mtu huyo aliyekuwa amevalia kifaa cha kujikinga dhidi ya gesi aliingia ndani ya ukumbi huo na kurusha gesi ya kutoa machozi. Pindi gesi ilivyojaa kwenyen ukumbi huo mshukiwa akaanza kuwafyatulia waliokuwemo risasi.Polisi wanasaema kuwa walimtia mbaroni mtu mmoja katika eneo la kuegesha magari karibu na eneo la tukio.
VIONGOZI WA UMMA WATAKIWA KUBADILI MTINDO WA KAZI ILI KUFIKIA DIRA 2050*
-
SERIKALI imesema hakuna tena biashara ya kawaida kwa Taasisi, Mashirika ya
Umma na Wakala za Serikali. Waziri Prof. Kitila Mkumbo amesema viongozi
lazim...
3 hours ago


No comments:
Post a Comment