Rais
Hu Jintao, Uchina ameziahidi serikali za Afrika mkopo karibu dola za
Marekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.Amesema kuwa
mkopo huo utasaidia katika ujenzi wa miundo mbinu, kilimo na maendeleo
ya biashara.
Rais
Jintao aliyasema hayo wakati wa mkutano wa ushirikiano baina ya Uchina
na viongozi wa Afrika mjini Beijing.Kuanzia barabara mpya za mjini
Nairobi hadi wauza kuku katika soko la Zambia ni dhahiri kwamba Uchina
imeweka nyayo zake katika kuinua uchumi wa Mataifa mengi barani Afrika.
Miundo
mbinu ni mojawapo ya sehemu ambazo Uchina imewekeza vilivyo barani
Afrika.Biashara kati ya Bara Afrika na Uchina imeongezeka kutoka dola
bilioni 10 miaka kumi iliyopita na kufikia takriban dola bilioni mia
moja na sitini hii leo.
Nchi hiyo imetoa mikopo zaidi kuliko Benki ya Dunia
No comments:
Post a Comment