Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 2, 2012

DR. HARRISON MWAKYEMBE AFANYA ZIARA YA KUKAGUA KIWANJA CHA NDEGE CHA ARUSHA NA BAADAE KUZINDUA BODI YA WAJUMBE WA KADCO



Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania Eng. Suleiman s. Suleiman akiwa na Mh. mwakyembe wakati alipofanya ziara ya kukagua kiwanja cha ndege cha Arusha na kilimanjaro na baadae kuzindua bodi ya ushauri ya KADCO.
akitoa maelekezo kwa Mheshimiwa Waziri wa Uchukuzi dr. mwakyembe,Eng. Suleiman alisema kuwa kiwanja hicho cha arusha kilisimama kupokea ndege kubwa kutokana na ukarabati uliokuwa ukifanyika wa barabara ya kuruka na kutua ndege ambao kwa sasa umekamilika na shirika la ndege la Precision litaanza kutua kiwanjani apo kuanzia mwanzoni mwa July 01 2012.
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege alieleza kuwa, mamlaka ya viwanja vya ndege katika mipango yake ya muda mfupi inatarajia kujenga maegesho mapya ya ndege,kujenga jengo jipya la abiria,kurefusha barabara ya kutua na kurukia ndege ili ifikie urefu wa meta 1800 na upana wa meta 30 na kujenga barabara ya kiungio yaani parrarel tax way.

No comments:

Post a Comment