HISPANIA jana waliifunga Italia 4-0
katika fainali ya Euro 2012 na watu wanasema ni kipigo kikali, lakini
mbele ya Ruvuma ni cha mtoto tu.
Ruvuma imethibitisha kuwa mwiba mkali
katika michuano ya Copa Coca-Cola mwaka huu baada ya leo asubuhi (Julai
2 mwaka huu) kuishushia Lindi kipigo cha mabao 7-2.
Hadi
mapumziko kwenye mechi hiyo ya kundi A iliyochezwa Uwanja wa Nyumbu
mkoani Pwani, washindi ambao kwa matokeo hayo wamejiweka katika nafasi
nzuri ya kucheza 16 bora walikuwa mbele kwa mabao 3-0.
Waliotikisa nyavu ni Anthony
Christian dakika ya 23 na 50, Edward Songo dakika ya 27, 75 na 86 na
Sunday Leonard dakika ya 32 na 60. Mabao ya Lindi yalifungwa na Salum
Mnyamwile dakika ya 18 kwa njia ya penalti na lingine dakika ya 48
kupitia kwa Mwarami Maundu.
Nayo Tanga imepata ushindi wake wa
kwanza katika michuano hiyo baada ya kuifunga Manyara mabao 2-0 katika
mechi ya kundi B iliyochezwa Uwanja wa Tamco mkoani Pwani. Mabao ya
washindi yalifungwa na Mbwana Musa dakika ya 47 na Issa Mwanga dakika ya
60.
Katika mechi tatu zilizotangulia
Tanga ilitoka sare ya mabao 3-3 na Morogoro, ikapata sare nyingine ya
1-1 dhidi ya Mwanza, na baadaye 1-1 na Tanga.
Kagera imeendelea kujitutumua katika
michuano hiyo baada ya kupata ushindi wake wa pili katika kundi D kwa
kuilaza Kusini Unguja bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa
Tanganyika Packers ulioko Kawe jijini Dar es Salaam.
Bao lake lilifungwa dakika ya 76 na
Novati Sebastian. Mechi iliyopita Kagera iliifunga Tabora mabao 2-0
baada ya kuteleza katika mechi mbili za kwanza kwa kufungwa na
Kilimanjaro na Singida.
Mechi nyingine ilichezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambapo Kinondoni iliibuka na ushindi
wa mabao 3-1 dhidi ya Mara.SOURCE BIN ZUBERY
No comments:
Post a Comment