Baada
ya tetesi za majuma kadha, serikali ya Uganda na Shirika la Afya
Duniani, WHO, wamethibitisha kuwa ugonjwa wa Ebola umeibuka magharibi
mwa nchi
Watu
kama 13 wamekufa na wengine kadha wanauguwa ugonjwa huo katika wilaya
ya Kibaale. Chanzo cha ugonjwa huo safari hii kingali kinachunguzwa.
Virusi
vya Ebola havina dawa wala chanjo ya kinga, na kati ya ishara zake ni
homa, kutapika, na kuhara.Ugonjwa huo ulizuka Uganda miaka 12 iliyopita,
na kuuwa watu zaidi ya 200.
Chanzo:http://www.bbc.co.uk/swahili/habari
No comments:
Post a Comment