HALMASHAURI
ya Jiji la Mbeya, kupitia Baraza la Madiwani limewafukuza kazi
watendaji sita, wakiwemo watumishi watatu wa Idara ya Uhasibu kwa
tuhuma za kujipatia fedha isiyo halali kiasi cha shilingi milioni
35,328,314.
Watumishi
waliokabiliwa na tuhuma hiyo ni Sarah Kibona Mhasibu mwandamizi,Tito
Robart Mwakisole Mhasibu daraja la kwanza pamoja na Petro Ulamso Yohana
ambaye ni mlinzi.
Akitoa
tamko la kuwafukuza kazi , Meya wa Jiji la Mbeya Athanasi Kapunga,
kwenye kikao cha Baraza la Madiwani mara baada ya kukaaa kama Kamati ya
kuwajadili watumishi hao, Baraza limependekeza kufukuzwa kazi kwa
watumishi hao.
Alisema,
Sara Kibona pamoja na Tito Robert wanakabiliwa na shitaka (kanuni 42)
kujipatia fedha isiyo halali (wizi)kiasi cha shilingi milioni
35,328,314.94 na shitaka la pili (kanuni ya 42) kushindwa kutimiza
wajibu au kutekeleza maelekezo aliyopewa na mwajiri wake wa kazi na
hivyo kusababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Alisema,
watuhumiwa wote wanadaiwa kutumia fursa ya cheo chao kwa kushirikiana
na mtumishi wa Benki ya NMB kuiba fedha za mishahara ya watumishi
wasiostahili kulipwa kwa kuingiza mishahara hiyo kwenye akaunti za watu
mbalimbali pamoja na za kwao wenyewe.
Aidha,
Meya huyo alisema kuhusu mlinzi Petro Ulamso yeye akaunti yake inadaiwa
kutumiwa na wahasibu hao kwa kuingiziwa fedha shilingi milioni
3,875,350 ambazo ni mali ya mwajiri.
Pia
mlinzi huyo anakabiliwa na shitaka la pili la kushindwa kutimiza wajibu
akiwa kama mlinzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya na kushindwa kutoa
taarifa ya kuingizwa kwa kiasi hicho cha fedha isivyo halali kwa mwajiri
ili zirejeshwe serikalini.
Baraza
hili limependekeza kufukuzwa kazi kwa mthamini ardhi daraja la kwanza
Joseph Ndaki kwa tuhuma za kughushi taarifa za uthamini wa ardhi ili
kuidanganya serikali kwa kusudio la kujipatia manufaa binafsi kutokana
na fedha ya zaidi ambayo ingelipwa kama fidia ya eneo la Ikuti na Inyala
kwa ardhi na mali ambazo hazipo.
pia
mtumishi huyo anadaiwa kushindwa kutimiza wajibu akiwa mtumishi wa
umma, kuharibu taswira ya utumishi wa umma mbele ya jamii na kufanya
vitendo vinavyodhalilisha utumishi wa umma ukishirikiana na wananchi
wasio waadilifu kughushi taarifa na pia kudhalilisha mamlaka ya
halmashauri ya jiji la Mbeya.
Alisema,
Ndaki alikuza eneo la uthamini pasipo uhalali na kwamba hekta 72 ndizo
alipaswa kuzifanyia kazi lakini yeye aliingiza hekta 190 kwa maslahi
yake mwenyewe na hivyo baraza limependekeza afukuzwe kazi.
source http://mbeyayetu.blogspot.com |
No comments:
Post a Comment