NDOTO kufunga pingu za maisha
siku za karibuni alizokuwanazo nyota kutoka 'Bongo move' Hemed Suleiman
'PHD', zimeota mbawa kufuatia wazazi wa mlimbwende aliyetaka kumuoa
kuweka ngumu.
katika mahojino mawili matatu
Hemed amesema kuwa tayari alikuwa ameanza taratibu za kushughulikia ndoa
yake na mrembo huyo iliyopangwa kufungwa kimya kimya kwa kuogopa watu
wenye nia mbaya lakini amejikuta akilazimika kustisha harakati hizo
kufuatia wazazi wa binti huyo wakaweka ngumu kwa madai kuwa wanataka
mtoto wao amalize kwanza masomo yake na kupata 'mastaz' kwa kuwa elimu
ya Degree aliyonayo hivi sasa wanahisi bado haijamtosha.
"unajua mchumba wangu hivi sasa
ana elimu ya degree hivyo wazazi wamesema hawezi kuruhusujambo hilo
kwanza mpaka apate 'mastaz' halafu ndiyo mambo mengine yatafuata,
imeniuma sana kwa kuwa wenyewe tulishakubaliana na mwenzangu alikuwa
tayari kwa hilo" alisema Hemed.
katika hatua nyingine
Hemed amesema kuwa yuko katika hatua za mwisho kutoa muvi yake mpya
aliyoibatiza jina la Mererani ndani yake akiwa amemshirikisha swahiba
wake wa kitambo Yusuf Mlela sambamba na wakali wengine kibao wanaofanya
kweli na Bongo move
STORI NA DISMAS TEN 0718489260


No comments:
Post a Comment