Mkali
wa soka kutoka Brazil ambae ni mwezi umepita toka aondoke kwenye club
ya Flamengo aliyokua anaichezea kutokana na kushindwa kumlipa mishahara
yake, amepatwa na tatizo jingine kwenye moja kati ya madili yake.Kampuni
ya vinywaji ya Coca-cola imeukatisha mkataba mnene na mchezaji
Ronaldinho baada ya mchezaji huyo kuonekana akiwa na vinywaji vya Pepsi
pembeni wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na club
yake mpya ya Atletico Mineiro.Mkataba
wake na Coca-cola ambao hauna hata mwaka toka usainiwe, ulitakiwa
kwenda mpaka 2014 ambapo malipo yake kwa mwaka ni dola za kimarekani
zaidi ya laki saba.Pepsi
ni wadhamini wa club yake mpya ya Mineiro na kuwepo kwa vinywaji hivyo
kwenye mkutano huo na waandishi wa habari sio chaguo au uamuzi wa
Ronaldinho, ni maamuzi ya club kwa sababu ndio yenye mkataba na Pepsi na
sio Dinho. na milladayo
WAHITIMU 417 KUTUNUKIWA VYETI MAHAFALI YA 17 YA CHUO CHA KODI NOVEMBA 22,
2024
-
MKuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Profesa Isaya Jairo akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 20, 2024 wakati wa kutangaza
siku ya ...
30 minutes ago
No comments:
Post a Comment