Hasheem Thabeet, Mtanzania anayecheza mpira wa kikapu Marekani amesaini mkataba wa miaka 2 na timu ya Oklahoma City Thunder..!!!
Watanzania ni wakati sasa wa kujivunia mafanikio ya baadhi ya watanzania wanaofanya vizuri katika viwango vya kidunia, katika historia ya michezo tangu tupate uhuru ni Hasheem Thabeet pekee ndio ameweza kufanikiwa na kucheza ligi ya juu kabisa duniani katika michezo.
Wako
watanzania wengi wamefanikiwa katika michezo mbali mbali na kufanikiwa
kucheza katika ligi za michezo mbali mbali na katika nchi mbali mbali
ila kila mchezo una ligi zake ambazo ni za kiwango cha juu juu kabisa
ni yeye pekee ndio amweza kufanya hivyo kwa kufanikiwa kucheza
mfululizo. Hasheem amecheza timu za Memphis na baadae kucheza Houston
Rockets na mwshoni mwa msimu uliopita alicheza Portland Trail Blazers.
Katika timu ya Blazers alicheza michezo yote 16 liyokuwa imebaki kabla
ya msimu kumalizika.
Hasheem
kwa sasa ndio mwafrika mwenye kiwango cha juu kabisa miongoni mwa
waafrika wanaocheza kikapu Marekani na ni mchezaji pekee anayecheza huko
toka ukanda wa Afrika , Mashariki, Kati na Kusini. Hasheem ni mchezaji
wa Afrika ambaye ameingia NBA akiwa na kiwango cha juu kabisa katika
historia ya mchezo huo, yaani No. 2 NBA Draft ya 2009.
Kwa
Hasheem kuchukuliwa na timu kama Oklahoma City ambao ni mabingwa wa
kanda ya magharibi ya NBA na mwaka huu walicheza fainali ya ubingwa wa
NBA na kushindwa na Miami Heat, inaonyesha jinsi ambavyo bado mchezaji
huyo anathaminiwa na bado uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kubwa kama OKC
ili iweze kufikia malengo yake.
Hivyo
basi kwetu sisi Tanzania tunampongeza na kujivunia mafanikio hayo.
Hasheem pia amekuwa ni mchezaji pekee wa kiwango cha juu ambaye amekuwa
akirudisha fadhila nyumbani na kila anapopata mapumziko huwa anarudi
nyumbani kuja kushirikiana na watanzania wenzake ili kuwainua na kuibua
vipaji.
Kwa
niaba ya shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, natoa pongezi nyingi
kwa Hasheem na tunamtakia kila heri na tumuombee kwa Mungu ili afanikiwe
zaidi katika kikapu.
Mungu Mbariki Hasheem, Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
Phares Magesa
Makamu wa Rais
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF)
No comments:
Post a Comment