Watanzania waliokuwa wakiishi ukimbizini Mogadishu Somalia wakirejea
nchini jana na ndege ya Umoja wa Mataifa wakiwa na familia zao
walikokuwa wakiishi tangu Januari 2001 wakikimbia vurugu zilizotokea
Zanzibar baada ya Uchaguzi Mkuu, Watanzania hao ni 38 wakiwa pamoja na
wake zao, Raia wa Somalia pamoja na watoto(Picha na Juma
Mohammed,MAELEZO Zanzibar)
Baadhi ya Wanzania 38 waliokuwa wakimbizi Jijini Mogadishu wakielekea
sehemu ya mapokezi mara baada ya kushuka katika ndege la Umoja wa
Mataifa iliyowaleta nyumbani wakiwa na wake zao walioa nchini Somalia
baada ya kuishi huko kwa miaka 11,walikimbia vurugu za Januari 26/27
mwaka 2001(Picha na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar)
Baadhi ya Watanzania waliokimbilia Mogadishu mwaka 2001 wakiwa katika
Ofisi ya Uhamiaji Zanzibar jana. Wa kwanza ni Mohammed Adam(38) akiwa
amembeba mwanawe mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Abeid Amani Karume,wanaotazama kamera ni baadhi ya wake wa Watanzania
hao ambao ni raia wa Somalia waliowasili jana wakitokea Mogadishu
Somalia na ndege ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia huduma za
kibinadamu(Picha na Juma Mohammed,MAELE Zanzibar)
Baadhi ya Watoto wakiwa na wazazi wao Raia wa Tanzania waliokuwa
wakimbizi nchini Somalia wakiwa katika Ofisia za Uhamiaji uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mara baada ya kuwasili na ndege
la UN zinazohusika na huduma za kibinadamu.(Picha na Juma
Mohammed,MAELEZO Zanzibar)
Baadhi ya akinamama Raia wa Somalia ambao wameolewa na Watanzania
waliokuwa ukimbizini Mogadishu wakifurahia jambo walipowasili uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,hapa walikuwa wakisubiri
taratibu za Uhamiaji(Picha na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar)
Watoto ambao kwa sasa ni Raia wa Somalia wakiwa na wazazi wao Raia wa
Tanzania waliokuwa wakimbizi nchini Somalia wakisubiri taratibu za
Uhamiaji katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume jana
baada ya kuwasili wakitokea Mogadishu na ndege ya Umoja wa Mataifa chini
uangalizi wa UNHCR(Picha na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar)
Watanzania waliokuwa wakimbizi katika kambi ya Mogadishu wakielekea
kupanda mabasi maalum yaliyoandaliwa na Shirika la kuhudumia wakimbizi
la Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume jana(Picha na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
No comments:
Post a Comment