Unakumbuka
February 8 2012 wakati baraza la mitihani lilipotangaza matokeo ya
kidato cha nne? stori kubwa ilikua mwanafunzi alieamua kuandika mistari
ya bongo fleva kwenye sehemu ya kujibia maswali.
“nashukuru
sana wanaosahihisha mitihani hii ya shule yangu, nitakapofeli naendelea
na fani yangu ya bongofleva, Majita wangu wako levo za juu na sio East
Zuu, kukosa ni kawaida kwa binadamu” hiyo ilikua ni swali namba 6 na 7
kwenye
swali la 11 kwenye moja ya mitihani yake aliandika mistari ya
bongofleva kwamba “acha utani my girl, unakuja nyumbani umezizi mwenzako
huku naona sijiwezi, kazi hiyo ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua
mzuri lakini mwisho ukawa mbaya”
Baada
ya hayo matokeo watu wengi ana walitamani kumfahamu huyu mwanafunzi,
Jina lake la kuzaliwa ni Julius lakini la kisanii ni Elinaja, na ametoa
sababu 5 za kwa nini aliamua kuandika hiyo mistari ya bongo fleva kwenye
mitihani yake ya kumaliza kidato cha nne.
Amesema
“1 ni kutaka kutuma ujumbe kwa watu wanaosimamia Elimu kwa ujumla,
sababu ya pili ni kutaka kusaidia watu wanaoteseka mtaani ambao wanaishi
maisha magumu kwa sababu tu ya kushindwa kwendana na system ya elimu
iliyopo ambayo ukishindwa kwenda nayo sawa umefeli, tulivyoumbwa kuna
mtu anaweza akawa anashindwa kitu flani lakini ni mzuri kwenye kitu
kingine sasa mfumo uliopo hautoi nafasi kwa wasioweza hiyo system,
sababu ya tatu ni kutokana na utaratibu wa usaishaji wa mitihani kwa
sababu sijui kama kuna mwanafunzi yeyote aliewahi kufanya mtihani wake
wa mwisho alafu mtihani wake ukarudishwa ili kuona wapi alipokosa na
wapi alipopata”
“Sababu
ya nne ni kuhusu wazazi kutambua uwezo wa watoto wao toka wakiwa wadogo
kipi wanaweza kipi hawawezi ili kuokoa muda na pesa, sababu ya tano ni
kwa serikali ijaribu kuweka shule za vipaji toka mwanafunzi akiwa mdogo
kabisa, leo hii kuna mtu amepata degree pale chuo kikuu kasoma miaka
mitatu na kupewa degree ya sanaa lakini hawezi kukuonyesha cheti hata
kimoja kwamba alikua na elimu ya awali ya hiyo degree, huwezi kuniambia
una degree wakati hukupata elimu ya msingi ya ulichosomea”
“Kwa
namna moja au nyingine sidhani kama nimefanikiwa kwa sababu
nilichofanya watu walikichukulia tofauti sikufanikiwa ndio maana
nimeamua kujitokeza kumalizia kazi ambayo niliianza kuifanya kule kwa
sababu nafsi yangu ilikua inanisuta, ila kwa sasa watu watakua wameelewa
na ninaweza kuwasaidia watu wengine” – Julius (Elinaja). na millad ayo
SOURCE MILLARD AYO

No comments:
Post a Comment