Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa yetu
JOKETI
Joseph (20) ameibuka kuwa mrembo wa mkoa wa Rukwa (Redd’s miss Rukwa
2012) katika mashindano yaliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa
Bomani uliopo mjini Sumbawanga.
Joketi
ambaye pia ni mkazi wa mjini hapa, aliwashinda washiriki wenzake tisa
kwa kushika nafasi ya kwanza katika kinyang’anyiro kilichojaa ushindani
wa kila aina.
Jaji
mkuu wa shindano hilo, Ismail Mpagama, alimtangaza mrembo huyo kuwa
mshindi wa kwanza, nafasi ya pili ikienda Asia Abdalah (19) na mshindi
wa tatu alikuwa Vency Edward (18).
Hata
hivyo katika shindano hilo, ilionekana dhairi kwamba Joketi ataibuka
na ushindi kwani alikonga nyoyo za watu waliojitokeza ambapo kila
alipopita jukwaani alishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza
kwenye ukumbi huo .
Kwa
mujibu wa muandaaji wa shindano hilo, Mariam Amri mshindi wa kwanza
ajipatia zawadi ya Seti moja ya Tv na dish kutoka kampuni ya Zuku
sambamba fedha taslimu Sh 300,000, mshindi wa pili akijivunia Sh 200,000
na watatu akiweka kibindoni Sh 170,000 washindi wa nne na tano
walijipatia Sh 120,000 kila mmoja huku washiriki wengine watano
wakiambulia kifuta jasho cha Sh 100,000.
Muandaaji
huyo aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kusaidia kufanikisha
mashindano hayo huku akiahidi kuwa washindi hao watawakilisha vema
katika mashindano yajayo ya kanda ya nyanda za juu kusini na yale ya
Redd’s miss Tanzania 2012 ngazi taifa.
Baada
ya kuibuka na ushindi Joketi alisema kuwa atajitahidi kadri awezavyo
kuibuka na ushindi katika mashindano ya kanda na kupata tiketi ya
kuingia katika ngazi ya kitaifa ambako nako ametamba kushinda na taji
hilo kwenda Rukwa safari hii.
SOURCE RUKWA YETU
No comments:
Post a Comment