.........................................................................................................................
JESHI la Polisi nchini, limesema linaendesha uchunguzi wa madai yaliyotolewa
hivi karibuni na Wakili Mwandamizi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando, kuwa kuna mtambo wa kunasa
mawasiliano ya simu za mikononi umeingizwa nchini kinyemela.
Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Msemaji jeshi hilo, Advera Senso, alisema baada ya madai hayo kutolewa wiki iliyopita, jeshi hilo, kupitia Kitengo cha Simu na Ufuatiliaji, limeanza kazi ya kuchunguza ukweli wa mashine hiyo na kama kweli kuna aliyefanya kitendo hicho hatua kali sana zitachukuliwa.
“Taarifa za kuwapo na mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu ya mtu mwingine zimetufikia, tunachunguza kwa ukaribu, tunajua suala hili lilianzia bungeni na sasa lipo ndani ya jamii.
“Kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine bila ridhaa yake ni kosa la jinai, sasa tusianze kuhukumu kitu ambacho hatuna uhakika nacho, tusubiri kazi ya uchunguzi ikamilike,” alisema Senso.
Hata hivyo, alivyotakiwa kueleza ni kwa nini kumekuwapo na uundaji wa kamati nyingi za uchunguzi wa matukio yanayojitokea pasipokuwa na mrejesho wake kwa jamii, Senso alisema matukio ya uchunguzi hufanywa pole pole ili kutoa majibu ya uhakika.
Aliwataka wananchi kuwa na imani ya Jeshi la Polisi, kwani limejipanga kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kuliongoza, licha ya kuwapo na kasoro ndogondogo.
......Source:Mtanzania...

No comments:
Post a Comment