!
Kwa
mara ya kwanza kifaa cha kujipima iwapo mtu ana virusi
vinavyosababisha ukimwi kimeidhinishwa na wataalam wanaodhibiti sekta
ya Afya nchini Marekani.
Kifaa hicho kwa jina OraQuick kitawezesha watu kutumia mate kuchunguza kama wana virusi vya ukimwi.
Itachukua muda wa kati ya dakika 20 na 40 kubaini matokeo ya uchunguzi huo.
Kifaa
hicho ambacho kitawezesha mtu kuchunguza hali yake mwenyewe nyumbani
au kokote anakotaka kitaanza kuuzwa nchini Marekani mwezi Oktoba mwaka
huu.
Serikali
ya Marekani inatarajia kuwa kifaa hicho kitasaidia kupunguza
maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kubadili tabia miongoni mwa watu
wanaoishi na virusi bila kujua.
Inakadiriwa kuwa robo millioni ya Wamarekani wako katika kitengo hicho.
Utafiti
wa kimatibabu unaoyesha kuwa majaribio ya matokeo ya uchunguzi wa
kifaa hicho cha Oraquick yananaweza kuwa sahihi kwa asilimia tisini na
mbili, miongoni mwa watu wanoishi na virusi vya ukimwi.
No comments:
Post a Comment