Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas akionyesha baadhi ya simu walizokutwa nazo majambazi hao
Simu walizokutwa nazo majambaz hao ikiwa ni sehemu ya vitu walivyokamatwa navyo
MAJAMBAZI YANAYOTEKA MAGARI BARABARANI YATIWA MBARONI
Iddi Uwessu-Arusha yetu blog
Jeshi
la polisi Mkoani Arusha limefanikiwa kuwatia mbaroni watu sita
watuhumiwa wa ujambazi,ambao inasadikiwa wamekuwa wakijihusisha na
matukio ya utekaji wa magari na uporaji wa mali za abiria katika mikoa
ya Mwanza, Dar es Salaam na Arusha
Operesheni
kali maarufu kama safishasafisha iliyoanzishwa na jeshi la polisi
mkoani Arusha kuanzia Juni 6 mwaka huu,ndiyo imefanikiwa kuwanasa
watuhumiwa hao kutoka mikoa ya Mwanza,Arusha,Mara na Dar es
Salaam,wakiwa na lundo la simu za mkononi ambazo zimeporwa kutoka kwa
raia katika magari waliyoyateka.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas,pamoja na
watuhumiwa kukutwa na simu 15 za aina mbalimbali,pia waliwaongoza polisi
hadi kwa mtu mwingine ambaye hununua simu zote wanazopora na mali
nyinginezo.
Miongoni
mwa watuhumiwa hao ni Joseph Kisaka Mahochi, mkazi wa Tabata Dar es
Salaam na Alexander Kitenge Malongori mkazi wa Nyakato Buzuruga jijini
Mwanza,ambapo watuhumiwa wengine wanatokea mkoani Arusha.
Kamanda
Sabas anasema operesheni hiyo imesaidia angalau kulifanya jiji na mkoa
wa Arusha kuwa shwari kwa kuwa tangu kuanza kwa operesheni
hiyo,watuhumiwa wapatao ishirini wanaosadikiwa kuwa majambazi wakubwa
wamenaswa na polisi,huku baadhi yao wakisafirishwa katika mikoa
mbalimbali kujibu tuhuma za makosa waliyoyafanya katika mikoa hiyo.
No comments:
Post a Comment