|
Manji anaondoka TFF, umati ukimsindikiza |
|
Sura za huzuni; wanachama wakisikitika nje ya ofisi za TFF |
|
Wanachama wakisikitikia pingamizi la Manji |
|
Ni huzuni tupu |
|
Hakuna anayufurahia |
|
Kila mtu ana hasira |
|
Yaani watu wamekasirika ile mbaya |
|
Hadi akina mama wana hasira pia |
|
Manji anatoka chumba cha mahojiano |
|
Anaziacha ofisi za TFF |
|
Anapotea |
|
Anawasalimu wazee |
|
Anajadiliana na wazee |
|
Umati unamsindikiza |
|
Anafunguliwa mlango wa gari lake |
|
Anaingia na kupotea |
MAMIA
ya wanachama wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, leo wameandamana hadi
makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Jijini kupinga
pingamizi alilowekewa mgombea Uenyekiti wa klabu hiyo katika uchaguzi wa
Julai 15, mwaka huu, Yussuf Manji.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Deo Lyatto leo ilikuwa
inapitia pingamizi mbili walizowekewa wagombea, Manji na Stanley Kavela
‘Yono’ anayewania Umakamu Mwenyekiti.
Tangu
saa nne asubuhi hadi saa nane mchana, Kamati hiyo ilikuwa inamuhoji
Manji ambaye hata alipotoka, ilielezwa alitakiwa kurejea tena.
Manji
alitoka mara mbili na kurejea kufuata vielelezo alivyotakiwa
kuwasilisha kuhusiana na pingamizi alilowekewa, ambalo vyanzo vinasema
ni zito.
Tangu
asubuhi wanachama walikuwa ‘kibao’ nje ya Ofisi za TFF, zilizopo ndani
ya Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam wakionyesha hasira zao dhidi
ya pingamizi hilo, ambalo aliloliweka anafanywa siri.
Wanachama walisikika wakisema kwamba kama Kamati ya Lyatto itamuengua Manji basi hakuna haja ya uchaguzi.
Miongoni
mwa waliokuwapo katika wanachama ni wazee wa klabu hiyo, akina Ibrahim
Akilimali, Dk Idrisa Katundu na wengineo, wakiwemo wanachama maarufu.
Kuna
kila dalili kwamba uamuzi wa kumuengua Manji katika uchaguzi huo
litakuwa jambo la hatari kwa klabu hiyo, kwani wanachama tayari
wamekwishajenga imani kubwa juu yake.
Manji
mwenyewe alipotoka kwenye chumba cha mahojiano alionekana asiye na
furaha hali ambayo ilizidi kuwatia wasiwasi wanachama kwamba huenda
kikao hakikuwa kizuri kwake. source bin zubery
No comments:
Post a Comment