Taarifa
kutoka Marekani zinaeleza kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani itaipatia
Kenya ndege nane ndogo zisizohitaji rubani, ikiwa ni sehemu ya msaada wa
kijeshi kwa nchi za Afrika Mashariki, ili kuzisaidia kupambana na
wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, al-Shabaab.
Gazeti
la Wall Street Journal la Marekani limearifu kuwa Kenya itapata ndege
hizo ambazo hazitakuwa na silaha, lakini zinaweza kugundua maeneo
yanayofaa kulengwa na ndege au majeshi ya ardhini.
Gazeti
hilo limesema ndege zisizokuwa na rubani ni sehemu ya msaada wa
Marekani, pamoja na malori, zana za mawasiliano, na silaha kwa Burundi,
Djibouti na Uganda.
No comments:
Post a Comment