Yusuf Manji.
MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, jaji mstaafu John Mkwawa,
amewataka viongozi wapya wa klabu hiyo kuhakikisha hawairudishi timu
hiyo nyuma.
Yanga, mwishoni mwa wiki iliyopita, ilifanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi za viongozi mbalimbali ikiwemo ya mwenyekiti iliyochukuliwa na Yusuf Manji, makamu mwenyekiti pamoja na nne za wajumbe wa kamati ya utendaji.
Kufuatia uchaguzi huo kukamilika kwa amani, Mkwawa ambaye kitaaluma ni mwanasheria, amewataka viongozi wapya ambao wanaongozwa na Manji, kuhakikisha timu hiyo hairudii makosa yaliyofanyika awali na kusababisha uchaguzi huo mdogo.
Mkwawa alisema viongozi hao wanatakiwa wajipange kuhakikisha Yanga inasonga mbele kwa kupanga mikakati kabambe ambayo ikitekelezwa itaweza kuisaidia timu hiyo kurudisha heshima yake ambayo ilianza kupotea kwa kupoteza makombe mbalimbali.
“Sisi kama kamati ya uchaguzi tumefurahi kuona uchaguzi huu umemalizika kwa amani, sasa ni kazi kwa viongozi wapya kuhakikisha Yanga haifanyi makosa kama yaliyotokea awali ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha uchaguzi huu,” alisema Mkwawa.
“Kama unakumbuka vizuri, Mei 24 ndiyo ilikuwa siku ya Nchunga kujiuzulu lakini hayo yote yanakuja kutokana na kitendo cha viongozi kushindwa kuonyesha uwajibikaji wao halisi, sasa ni ilani yetu kwao kuhakikisha wanajipanga kwa lengo ya kuiendeleza Yanga,” aliongeza.

No comments:
Post a Comment