Mfanyabiashara Sijali Nyomolelo enzi wa uhai wake akiwa Wodini baada ya kupata ajali ya pikipiki
Mjane Sophia Kilyenyi akielezea siri iliyofichika juu ya kiasi halisi cha fedha alizokuwa nazo mfanyabiashara huyo
Maandalizi ya mazishi nyumbani kwa marehemu eneo la Mwangata mjini Iringa mchana wa leo
Mdogo wa marehemu Sijali akiwa na mjane
IKIWA
ni siku moja toka ajali mbaya iliyosababisha kifo cha
mfanyabiashara wa maduka ya Nyama (Bucha) mjini Iringa Sijali
Nyomolelo kufa katika ajali mbaya ya gari katika eneo la Ikonongo kata
ya Mkwawa mjini Iringa, siri nzito imefichuku juu ya kiasi cha fedha
alizokuwa nazo.
Siri
hiyo imefichuka baada ya kuwepo kwa utata juu ya kiasi halisi
ambacho marehemu huyo alikuwa nacho katika gari yake aina ya Taxi
yenye namba za usajili T 150 AAM ,ambayo alikuwa akiiendesha kabla ya
kupata ajali mbaya jana majira ya saa 2 asubuhi .
Wakati
taarifa za awali zilidai kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa na kiasi
cha shilingi zaidi ya 500,000 katika gari yake na ndizo zilizoporwa
na vibaka waliofika katika gari hiyo kutoa msaada ,mjane wa marehemu
ameibuka na kuzungumza na mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa na
kiasi cha zaidi ya Tsh Milioni 6 katika gari lake .
Mjane
huyo Bi Sophia Kilyenyi ameyasema hayo leo wakati akiushukuru mtandao
huu kwa kufuatilia kwa kina ajali hiyo na kufichua yaliyofichika
ikiwa ni pamoja na kutoa picha ya video ambay0 ni kauli ya mwisho ya
marehemu akiwa hoi katika Hospital ya mkoa wa Iringa.
Alisema
kuwa fedha hizo alizichukua nyumbani kwa ajili ya kwenda kununua
ng'ombe katika kijiji cha Itamba ili kuweza kuzichinja kwa ajili ya
bucha zake tatu alizokuwa akizimiliki mjini Iringa.
Hata
hivyo mbali ya fedha hizo kuchukua nyumbani baadhi ya fedha
alimtuma kwenda kuzichukua kwa mmoja kati ya wafanyabiashara wa nyama
katika soko kuu la Manispaa ya Iringa ili kuongeza kwa kiasi
kilichokuwepo.
Hata
hivyo alisema bado hajatambua kiasi sahihi alichokuwa nacho kwani
kabla ya kuondoka asubuhi alipata kuzungumzia suala la kwenda benki
kuchukua fedha zaidi ili kuweza kwenda kesho kununua ng'ombe mnadani
Pawaga .
Huku
kuhusu gari alisema kuwa baadhi ya vitu viliporwa na vibaka hao
wakati vitu vingine katika gari hilo ambalo alipata nalo ajali
zimehifadhiwa sehemu salama.
Mfanyabiashara
huyo Sijali Nyomolelo ambaye pia alipata kupata ajali mbaya ya Piki
piki na kuvunjika mguu wake amezikwa leo katika Makabuli ya Kitwiru
mjini Iringa aeacha watoto watatu na mjane mmoja .
Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi Amina
CHANZO FRANCIS GODWIN
No comments:
Post a Comment