Mratibu na jaji wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012,Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali kutoka Clouds FM,akimpa maelekezo mafupi Pacha Great mara baada ya kuibuka kinara wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,kwa kuwashinda mahasimu wenzake wapatao 32 waliofika kushirika mchakato wa shindano hilo.shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa limeandaliwa na Prime Time Promotions/Clouds FM kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager. |
Majaji
wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa wakijadiliana
jambo,kutoka kulia ni JCB,Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali kutoka Clouds FM
pamoja na Mdau wa muziki wa hip hop,Mo-Plus.
Washabiki wakishangilia jambo ukumbini humo.
Mwanadada
mwingine aliyejitokeza kunogesha shindano la kumsaka mkali wa Serengeti
Fiesta Mc Shujaa,aliyejulikana kwa jina la Catrina akiimba kwa sauti
tamu kabisa na yenye kusisimua mashabiki jioni ya leo ndani ya Mawingu
Club,jijini Arusha.
Mratibu
wa shindano la kumsaka mkali wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa,Adam Mchiomvu
akitajana majina yaliyoingia fainali kwenye shindano hilo,ambalo
limekuwa na msisimko mkubwa kwa vijana wengi wa jiji la Arusha,katika
mchakato mzima wa shindano hilo walijitokeza vijana 32,wakachunjwa na
kupatikana wengine 12,na hatimaye kuwapata sita ambao walishindana
vikali,aidha katika sita hao aliihitajika kinara mmoja tu wa kughani kwa
miondoko huru.
Mwanadada
machachari kabisa aitwaye Tiger Eyes akionesha umahiri wake wa kughani
mbele mashabiki waliofika kwenye shindano la kumsaka mkali wa Serengeti
Fiesta Mc Shujaa
NA FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment