Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Suleiman Kova.
Na.MO BLOG TEAM
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja raia wa
Kenya kwa tuhuma za kuteka nyara na shambulio la kudhuru mwili dhidi ya
Dkt. Stephen Ulimboka lilifanyika tarehe 26 Juni 2012.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa
Polisi, Kanda Maalum Suleiman Kova amesema mtu huyo aitwaye Joshua Gitu
Mhindi mwenye umri wa miaka 31, ana kitambulisho cha utaifa Na.29166938
kilichotolewa Nyeri na hati ya kusafiria ya dharura Na.0123431
iliyotolewa Namanga Kenya.
Kamanda
Kova amesema katika mahojiano na polisi mtu huyo alieza kwamba yeye ni
mwanachama wa kikundi cha kihalifu kinachojulikana kama GUN STAR chenye
makao yake eneo la RUIRU wilaya ya Thika nchini Kenya na kudai kuwa
kinaongozwa na mtu mwenye jina la utani SILENCE akisaidiwa na PAST,
ambao wamekuwa wakifanya matukio mengi ya kihalifu nchini Kenya.
Mtu
huyo alipohojiwa zaidi alisema alikuja Tanzania na wenzake 12 kwa lengo
la kumdhuru Dkt. Stephen Ulimboka baaada ya kukodiwa na mtu ambaye
hakumtaja jina, ambaye anaamini kuwa ni mtumishi wa serikali.
Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wengine waliohusika.
CHANZO THIS DAY MAGAZINE
No comments:
Post a Comment