Manji akiwa amemuinua mkono Bin Kleb, wengine kulia ni Manyama na Nyambaya, wakati kushoto ni Sanga |
MGOMBEA
Uenyekiti wa klabu ya Yanga, katika uchaguzi wa Jumapili ukumbi wa
Diamond Jubilee, Dar es Salaam Yussuf Mehboob Manji leo ametambulisha
watu watano anaotaka kuchaguliwa nao wakati alipokuwa akihutubia mamia
ya wanachama kwenye Mkutano wa kampeni, Uwanja wa Kaunda, uliopo makao
makuu ya klabu, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.
Manji
aliwataja watu hao kuwa ni nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga
na Wajumbe wanne ni Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro, Lameck Nyambaya
na George Manyama.
Ikumbukwe
uchaguzi huo mdogo unafuatia Wajumbe wengi wa Kamati ya Utendaji
iliyochaguliwa miaka miwili iliyopita, akiwemo Mwenyekiti Wakili Lloyd
Baharagu Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha kujiuzulu na
watakaochaguliwa Jumapili watadumu kwa miaka miwili, kumalizia kipindi
cha uongozi cha waliojiuzulu.
Manji
aliwaomba wanachama wa Yanga pamoja na kumchagua yeye Jumapili, pia
wawachague na watu hao watano, Sanga, Katabaro, Bin Kleb, Nyambaya na
Manyama, kwani ni watu ambao anaamini atafanya nao kazi vizuri na kwa
ufanisi.
Alisema
iwapo akichaguliwa watu hao na mambo yakawa mabaya klabuni, atakuwa
tayari kujiuzulu lakini akasema atasikitika iwapo atachaguliwa pamoja na
watu tofauti nao hao.
Alisema
katika kipindi hiki ambacho klabu haina uongozi, watu hao watano
wamekuwa wakimsaidia kujenga timu kama kusajili na kadhalika kwa
kujitolea hivyo ana imani nao kwa kiasi kikubwa.
Shughuli
hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa wanachama Vijana wa Yanga, Bakili
Mohamed Makele na Mwenyekiti wa Wazee, Mzee Ibrahim Ally Akilimali,
ambao waliwaomba wana Yanga kuchagua timu hiyo na mambo yatakuwa mazuri.
Umati
wa wanachama wanaokadiriwa kufika 2000 au zaidi ulihudhuria mkutano huo
na wakati wote walikuwa wakishangilia hotuba, kuonyesha kwamba
wanaafiki.
Manji anahutubia |
Manji anahutubia |
Manji anahutubia |
No comments:
Post a Comment