Mechi
kati ya Simba SC na Express imemalizika Uwanja wa Taifa, kwa sare ya
bila kufungana. Timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha pili.
Ilikuwa mechi nzuri.
Amir Maftah akitibiwa na Dk Cossmas Kapinga baada ya kuumia
Jingo Suleiman wa Express, anaweza kuwa mchezaji mfupi zaidi Afrika Mashariki na kati kwa sasa
Kaimu Nahodha wa Simba, Uhuru Suleiman baada ya mechi
BIN ZUBEIRY na Mussa Mudde wa Simba
Mechi
ya kirafiki kati ya mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC na mabingwa wa
Uganda inaingia katika kipindi cha pili na timu na hizo hazijafungana.
Katika dakika 45 za kwanza, timu zimeshambuliana kwa zamu. Habari njema
ni kiungo Patrick Kanu Mbivayanga kutoka DRC, anacheza mpira wa hali ya
juu. Katika safu ya ulinzi, Masombo amesimama imara. Simba inacheza soka
ya kuvutia kwa kuonana. Imejaza viungo wengi Amri Kiemba, Shomary
Kapombe, Mussa Mudde, Mbivayanga na Uhuru Suleiman na wanafanya kazi
nzuri. Abdallah Juma, ambaye unaweza kusema Emmanuel Gabriel amerejea
Simba anawapa kazi mabeki wa Express, ingawa kipindi cha pili ametolewa.
Kipa Albert Mweta amefanya kazi nzuri na anajiamini mno.
|
No comments:
Post a Comment