Beki
wa Simba, Juma Nyoso (kulia) akiruka kuokoa mpira wa hatari mbele ya
mshambuliaji wa As Vita ya Congo,wakati wa mchezo wa kundi A, wa Kombe
la Kagame uliomaliika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. As Vita
ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kwa njia ya mkwaju wa penati katika
dakika ya 35 ambapo goli hilo lilifungwa na Etekiama Taddy. Simba nao
waliweza kusawazisha bao hilo katika dakika ya 66 kupitia mshambuliaji
wake Haruna Moshi 'Boban'.
Kiungo
mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba (kushoto) akichuana kuwania mpira
na beki wa As Vita, Mfongang Alfred, wakati wa mchezo huo.
Juma
Nyoso wa Simba (kushoto) akimchezea rafu mcheaji wa As Vita, Etekiama
Taddy, wakati wa mchezo huo leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa As Vita, Magola Mapanda (kulia) akiwania mpira na beki wa Simba, Juma Nyoso, wakati wa mchezo huo.
Kipa
wa Simba, Juma Kaseja, akichungulia mpira uliopigwa kwa mkwaju wa
penati na Etekiama Taddy na kuandika bao katika dakika ya 35 ya kipindi
cha kwanza. Simba wamekosa penati katika dakika za majeruhi baada ya
Sunzu kupiga fyongo na kuokolewa na kipa wa AS Vita na kufanya matokeo
kuwa 1-1.
YANGA KUCHEZA NA MAFUNZO, SIMBA NA AZAM
WAKATI
huo huo tayari Shirikisho la mpira wa miguu Tff, limekwishatoa maamuzi
kwa kurusha shilingi na kumpata mshindi wa kwanza na wa pili katika
kundi B, ambapo Yanga sasa itacheza na Mafunzo siku ya jumatatu na Azam
kuchea na Simba na As Vita watacheza na Atletico.
Picha na Sufiani Mafoto Blog
No comments:
Post a Comment