Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, July 12, 2012

SIMBA YATWAA UBINGWA WA URAFIKI CUP - YAIFUNGA AZAM KWA PENATI 3-2



SIMBA SC imetwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki, baada ya kuifunga Azam FC kwa penalti 3-1 usiku huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90. SOURCE BIN ZUBERY

Penalti za Simba zilikwamishwa nyavuni na Mwinyi Kazomoto, Amir Maftah na Kiggi Makassy, wakati Haruna Moshi Boban alipaisha na kwa upande wa Azam FC, aliyefunga ni Hamisi Mcha ‘Vialli’ pekee, wakati Samir Hajji Nuhu ilidakwa na Juma Kaseja, Ibrahim Mwaipopo ilipanguliwa na Himid Mao ‘iliota mbawa’.

Kabla ya matuta, mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Sunzu alitangulia kuifungia Simba dakika ya 29 kabla ya Hamisi Mcha ‘Vialli’ kusawazisha dakika ya 45 na ushei.

Kipindi cha pili mchezo ulichangamka zaidi na dakika ya 81, John Bocco ‘Adebayor’ aliyetokea benchi aliifungia Azam bao la pili, kabla ya Kazimoto kuisawazishia Simba kwa penalti dakika ya 87, baada ya Danny Mrwanda kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Kwa ushindi huo, Simba SC wamezawadiwa Sh. Milioni 10 na Azam FC Milioni 5.
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Sunzu (10) baada ya kufunga. 
Aggre Morris wa kwanza kushoto, John Bocco wakimpongeza Viallli (wa pili kushoto) kufunga la kusawazisha
Kikosi kilichoanza Azam
Kikosi kilichoanza Simba






No comments:

Post a Comment