MUUZA sura anayetamba kwenye video za Kibongo, Agness Jerald
‘Masogange’ juzikati alinusurika kuaga dunia baada ya kuchanganya pombe
na dawa aina ya Cephalaxin kutokana kuudhiwa na mpenzi, Risasi Jumamosi
lina habari kamili.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Masogange aitwaye Janneth asubuhi
ya siku ya tukio, Agness alimpigia simu na kumtaka afike nyumbani kwake
kwa kuwa tumbo lilikuwa likimsumbua.
Hata hivyo, Janneth alidhani rafiki yake huyo alikuwa akimtania, kwa
kufikiria kuwa alikuwa akimtaka tu afike nyumbani kwake na hakuwa na
tatizo lolote.
Jananeth alizidi kueleza kuwa baada ya muda alipigiwa tena simu na
Agness huku akilia ndipo alipohisi kuwa kulikuwa na kitu, akaamua kukodi
teski kwa ajili ya kumuwahi.
“Nilipofika nyumbani kwake nilikuta amejifungia kwa ndani, hivyo
ikabidi kuvunja mlango, nilipofanikiwa kuingia nilimkuta akiwa hoi,”
alisema Janneth.
Janneth alisema kuwa baada ya kuvunja mlango alimkuta Agness akiwa
amelala karibu na chooni na pembeni yake kukiwa na chupa ya pombe na
pakti ya dawa.
“Nilikwenda dukani na kumnunulia maziwa na kumnywesha kwa kuwa
nilihisi atakuwa amechanganya dawa na pombe, kisha nikamkimbiza katika
Hospitali ya Mama Ngoma kwa ajili ya matibabu.”
Baada ya kupata taarifa hizo na kuambiwa kuwa Agness alikuwa
amesharudi nyumbani kwake, mwandishi wetu alimfuata na kumkuta akiwa
amejilaza nje ya nyumba yake, hapohapo akamdodosa kwa maswali:
Risasi: Kuna hisia kuwa umekunywa pombe na kuchanganya na dawa?
Risasi: Kuna hisia kuwa umekunywa pombe na kuchanganya na dawa?
Agness: Ni kweli.
Risasi: Ulifanya kwa kudhamiria au?
Agness: Kwa kweli nilidhamiria.Risasi: Kisa hasa ni nini?
Agness: Ni mapenzi tu yanitesa.
Risasi: Vipi umesalitiwa au?
Agness: We acha tu,nitakueleza nikiwa vizuri.
Bado gazeti hili litaendelea kumdodosa Agness kisa kilichomfa kufikia hatua hiyo
DADA VP HUKO MBALL SUM YA NN
ReplyDelete