Katika
harakati za kuimarisha zoezi la ukataji tiketi za treni ya abiria
Menejimenti ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imetoa Mwongozo ufuatao:
TUNAPENDA
KUWAFAHAMISHA WATEJA WETU KWAMBA, KUANZIA JUMATATU JULAI 16, 2012
MTEJA YEYOTE ANAYETAKA KUNUNUA TIKETI YA TRENI LAZIMA AONESHE
KITAMBULISHO CHAKE KWA KARANI MUUZA TIKETI BILA HIVYO HATUTAWEZA
KUMHUDUMIA.
VITAMBULISHO
VINAVYOTAMBULIKA NI VIFUATAVYO; KITAMBULISHO CHA KUPIGIA KURA,
LESENI MPYA YA UDEREVA, KITAMBULISHO CHA MUAJIRI, HATI YA KUSAFIRIA,
KITAMBULISHO CHA SHULE, BARUA KUITOKA KWA MWENYEKITI WA SERIKALI YA
MITAA NAKADHALIKA UTARATIBU HUU MPYA NI KWA AJILI YA KUONGEZA UFANISI
NA KUBORESHA HUDUMA ZETU KWA WATEJA WETU!
IMETOLEWA NA MENEJA UHUSIANO ( MIDLADJY MAEZ) KWA NIABA YA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL MHANDISI KIPALLO AMAN KISAMFU
DAR ES SALAAM
JULAI 16, 2012
No comments:
Post a Comment