Chege amepata ajali maeneo ya Temeke Jana 16 July mida ya saa nne usiku. Ajali imesababishwa na mwendesha pikipiki ambaye alikuwa amelewa sana na ameiba pikipiki alio kuwa anaendesha.Mwenye pikipiki alifika hospitalini na kusema alikuwa akijitayarisha kuwasha pikipiki yake huku akiva koti kwa ajili ya kujizuia na baridi ndipo alipo sukumwa pembeni na mlevi huyo na kuibiwa pikipiki yake . Kwa mwendo wa kasi sana pikipiki hio iliingia barabarani bila kujali magari wala usalama.
Chege amepata maumivu makali kwenye mkono wake wa kushoto na ameshapata matibabu hospitali ya Kinondoni mida ya saa sita usiku.
Kabla ya ajali chege alikuwa studio akitayarisha CD Ya show atakayo kwenda kufanya Kigoma pamoja na kigoma All star tarehe 17 July 2012. Baada ya kutayarisha hio CD Alikuwa aje kinondoni kujitayarisha na safari yake ya Kigoma mapema asubuhi.
MUFTI MKUU TANZANIA KUJA NA ZIARA YA KUIMARISHA UONGOZI MKOA WA DODOMA
-
Mufti Mkuu Sheikh Abubakar Zubeir amesema Baraza limepanga kufanya ziara
rasmi mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kutembelea mikoa yote 26
nc...
8 hours ago
No comments:
Post a Comment