Apparently utamu wa Pepsi umemkosesha
dili lenye thamani ya zaidi ya Billioni 2 za kibongo mchezaji wa
kimataifa wa Brazil Ronaldinho Gaucho baada ya kampuni ya Coca-Cola
kumpiga chini kwenye kazi ya ubalozi baada ya kuonekana akitumia
kinywaji cha wapinzani wao kibiashara.
Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa akiwahesabu Coca-Cola kama moja ya makampuni mengi anayofanya nayo kazi kwa kumdhamini, lakini akufanya kosa la kuonekana akinywa kinywaji cha Pepsi wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.
Kiwango cha Ronaldinho tangu arudi Brazil na ugomvi wake na klabu ya Flamengo umekuwa ukimfanya atengeneze sana vichwa vya habari vya magazeti kwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.
Na kufuatia kwa kosa lake la hivi karibuni, Coke hawakuonyesha kusita katika kuukatisha mkataba wao na kiungo huyu mwenye miaka 32 na mchezaji bora wa dunia wa zamani wa FIFA.
"Kitendo cha kuonekana akinywa Pepsi kimeharibu taswira yake mbele ya wanywaji wa Coke. Watamuelewa vipi balozi anayewatangazia bidhaa hi halafu yeye anatumia nyingine. Kwa hili tumeamua kuuistisha mkataba wake na sisi." - alisema Mkuu wa masoko wa Coca-Cola Marcelo Pontes.

SOURCE SHAFFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment