Mtuhumiwa wa
wizi wa umeme Siwamini Muhammed, akiwa chini ya Ulinzi wa jeshi la
polisi na wakaguzi wa Shirika la umeme Tanesco baada ya nyumba yake
ilioko Mbagala kizuiani kukutwa ikiwa imeunganishwa umeme kwa njia ya
wizi kabla haujafika kwenye mita nakuutumia bila kuulipia.
Sehemu
iliyounganishwa umeme kabla haujafika kwenye mita na kusomwa kwenye moja
ya nyumba zilizokutwa eneo la Kizuiani Mbagala jijini Dar es Salaa
wakati wa Operesheni maalum ya kukamata wezi wa umeme linaloendelea
kwenye kanda ya Tanesco Temeke ambapo watu saba wameshikiliwa na jeshi
la polisi kwa wizi huo.
WATU saba wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi wa umeme baada ya kuwakamata kwenye operesheni ya kukamata watu wanaoiba umeme inayoendelea kwenye kanda maalum ya Tanesco Temeke.
WATU saba wanashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi wa umeme baada ya kuwakamata kwenye operesheni ya kukamata watu wanaoiba umeme inayoendelea kwenye kanda maalum ya Tanesco Temeke.
Kwenye
zoezi hilo ambalo linafanywa na timu maalum ya Tanesco na kusaidiana na
Jeshi la Polisi kumegundulika wizi wa aina mbalimbaliikiwemo
wakujiunganishia umeme kwa kupitisha waya chini ya aridhi na
kujiunganishia kabla haujafika kwenye mita na kusomwa.
Zoezi
hilo ambalo leo ilikuwa ni zamu ya eneo la Mbagala Kizuiani liliwapa
wakati mgumu wakaguzi wa mifumo ya umeme wa shirika hilo baada ya kufika
mtaa wa CCM eneo hilo la kiuzuiani na kukuta nyumba zaidi ya 6
wakitumia umeme kutoka kwenye nyumba moja huku wakiwa wamejiunganishia
kwa kuchumbia nyaya chini ya aridhi na wakaguzi hao kuamua kukata kabisa
waya zake na kuwashikilia watuhumiwa wa wizi huo.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo Meneja wakanda hiyo ya Temeke Richard Malaamia,
amesema tatizo la wizi nikubwa kwahiyo wanalazimika kufanya zoezi hilo
kuwa endelevu hadi wananchi watakapojenga mazoea kutumia umeme kwa
kufuata utaratibu.
Malamia amesema wisi wa umeme uekua ukisababisha hasara ya Tsh 89Millioni kwa mwezi na kulikosesha mapato shirika hilo.
Hata
hivyo wakaguzi wa mifumo ya umeme walimweleza mwandishi wa habari hizi
kuwa wao binafsi walidhani tatizo la wizi wa umeme lipo zaidi kwa
watumiaji wakubwa lakini kkutokana na matukio wanayoshuhudia inawapa
wasiwasi kuwa kuna idadi kubwa zaidi ya watu wanao iba umeme hata kwa
watumiaji wadogo kabisa.
Mkaguzi
Daniel Maswi alisema, tabia ya kujiunganishia umeme kabla ya kufika
kwenye mita ni hatari na inaweza kusababisha hatari hata ya kulipua
nyumba kwani nyaya zinazo tumika ni hafifu mno na umeme unaopita ni
mkubwa.

No comments:
Post a Comment