Zaidi
ya watu mia moja wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya lori
la mafuta kuanguka kusini mashariki mwa nigeria katika Jimbo la Delta.Wakuu
wa Serikali wanasema kuwa wenyeji wa eneo hilo walikimbilia kuzoa
mafuta yaliokuwa yakichuruzika toka lori hilo lakini likalipuka na na
kusababisha maafa hayo.
Mwandishi wa habari Emeka Idika ameiambia BBC kuwa mazishi ya halaiki
kwa watu waliofariki kutokana na moto na wasioweza kutambulika
yatafanywa katika Jimbo la Rivers wakati wengine wapatao 35 wamelazwa
katika hospitali.
Mwandishi huyo ameongezea kusema kuwa idadi ya vifo huenda
ikaongezeka kwa sababu kuna baadhi ya watu kutoka vijiji vilivyo karibu
na hapo Okogbe waliokua wamekumbwa na balaa la moto mkubwa walikimbilia
vichakani na miili yao bado haijaonekana.
Mwandishi mwingine , Oluchi Iwuoha Chimezie, ameiambia BBC kuwa alihesabu zaidi ya maiti 100.
Shirika la habari la Reauters limemnukuu msemaji wa Polisi ya Jimbo
la Rivers state, Ben Ugwuegbulam akisema kuwa "mapema leo Lori
lililobeba mafuta lilipinduka huko Okogbe na watu kukimbia haraka
kujizolea mafuta yaliyokuwa yakimiminika na ghafla bin vuu moto
ukalipuka na kusababisha madhara.
Taasisi inayosimamia usalama wa barabarani imesema kuwa Lori hilo
liligonga magari matatu. Matukio ya aina hiyo si mageni nchini Nigeria.
Mamiya ya watu wamefariki katika kipindi cha miaka kumi iliyopita
wakijaribu kuchota mafuta kutoka mabomba yanayovuja kwa sababu ya
kuvunjwa makusudi au watu wanaojaribu kuiba mafuta.
Nigeria ni nchi inayozalisha na kuuza mafuta kwa kiwango kikubwa lakini mamilioni ya raia wake wanaishi maisha ya ufukara.

No comments:
Post a Comment