NA KHADIJA KHAMIS –IDARA YA HABARI MAELEZO
Wizara ya Afya Zanzibar
imejipanga kutoa huduma zote za uzazi bure kwa wananchi zikiwemo zile
za upasuaji zitafanyika bila ya malipo kuanzia mwaka wa fedha 2012 na
kuendalea.
Hayo
yameelezwa leo huko katika ukumbi wa baraza la wawakilishi nje kidogo
na mji wa Zanzibar ,wakati akiwasilisha hotuba ya waziri wa afya mhe
juma duni haji kuhusu makadirio na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012
-2013
Alisema kuwa tamko hilo limetekeleza
azma ya kiongozi mkuu wa serikali ,rais wa zanzibar na mwenyekiti wa
baraza la mapinduzi ya kuhakikisha kuwa akinamama wote wanapatiwa huduma
ya uzazi bure .
Aidha alieleza kuwa mtu yeyote ambae
atatolezwa pesa katika huduma za kizazi ikiwemo kujifungua kwa njia ya
kawaida na upasuaji atoe taarifa kwa wizara husika ili aweze
kuchukuliwa hatua za kisheria .
Waziri huyo alitoa pongezi kwa rais wa
Zanzibar kwa uwamuzi wake wa busara kuweza kufuta michango yote ya
fedha kwa mama wajawazito .
Tamko hilo
lilitolewa tarehe 9/05/2012 lenye lengo la kuwapunguzia makali ya
maisha mama wajawazito, kupunguza vifo vya akinamama na watoto pamoja na
kutekeleza malengo ya millenia
Aidha
alisema kwamba katika kutekeleza mikakati wa kupunguza vifo vitokanavyo
na uzazi kwa akinamama huduma za kujifungua zinaendelea kuimarishwa katika hospitali zote za uzazi .
Amefahamisha
kuwa hadi hufikia mwezi machi 2012 waliweza kupokea wajawazito
waliolazwa katika hospitali ya idara ya tiba kwa unguja na pemba ni
8090kati ya wajawazito 6,075 walijifungua kwa njia ya kawaida na 395
walijifungua kwa njia ya upasuaji na akinamama 18 walifariki dunia na
jumla ya watoto 6,528 walizaliwa katika kipindi hicho.
No comments:
Post a Comment