Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, July 12, 2012

ZAIDI YA ASILIMIA 90%YA MADEREVA WA PIKIPIKI JIJINI ARUSHA HAWANA LESENI !!!



Mkijua sheria za usalama barabarani hata rushwa hamtatoa maana unajua sheria
Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani wa Arusha Marson mwakyoma akiongea na baadhi ya madereva wa pikipiki waliofuata pikipiki zao kituoni hapa ambazo zimekamatwa
ZAIDI ya  asilimia 90%  ya  madereva wa pikipiki mkoani Arusha hawana leseni za udereva na wengine hawajui sheria za barabarani
Hayo yamebainishwa na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa Marson Mwakyoma wakati akifanya mahojiano na libeneke la kaskazini ofisini kwake
Alisema kuwa kutokana na ajali nyingi ambazo zimekuwa zikitokea kikosi cha usalama babarbarani kimefanya uchunguzi na kubaini kuwa zaidi ya madereva hao wamekuwa hawana leseni na  ambao wanayo wamekuwa hawajapata kwakufata sheria   na wengine hawajasoma kabisa.

No comments:

Post a Comment