Leo nikiwa safari kutokea Dar es Salaam kwenda Arusha nimejihimu alfariji ila kufika Wami darajani saa moja asubuhi, nikakuta Gari aina ya Fuso lililokuwa limebeba mkaa limepata ajali ya kugonga kingo za daraja na kunusufika kutumbukia mtoni. Kwa mujibu wa utingo wa gari hilo, ajali hiyo ilitokea mida ya saa tano usiku wa jana, na chanzo cha ajali ni dereva kutokuwa makini maana alikuwa anawasha sigara ndipo balaa hilo likawakuta. Kwa mapenzi ya mungu wote walitoka salama.
Ajali hiyo ilisababisha mateso makubwa kwa watu waliokuwa wanatumia njia hiyo leo. Imechukua muda mrefu sana hadi gari hilo kuondolewa darajani na magari kuanza kuruhusiwa kupita ilipofika saa tano mchana, ambapo pande zote mbili kulikuwa na mamia ya magari na idadi kubwa sana ya watu.
Nadhani pangekuwa na madaraja mawili ingeweza kurahisisha kuondoa hadha kubwa kwa wasafiri. Jambo lingine ni Breakdown iliyokuwa inavuta gari hiyo kutokuwa na uwezo, jambo ambalo limesababisha kazi hiyo kuchukua muda mrefu sana.
Mdau wa Kigambonino
Watu Mbali mbali waliokuwa safarini leo kwa kutumia barabara hiyo wakiangalia taratibu ya kuondolewa kwa gari hilo lililokuwa limeanguka katikati ya daraja la Wami.
Msongamano wa magari unavyoonekana
picha na habari kwa hisani http://www.sophiakessy.com
No comments:
Post a Comment