Baadhi
ya wananchi wakiwa wanaangalia mwili wa marehemu ambaye amepoteza
maisha papo hapo mara baada ya kugongwa na lori na kukanyagwa kichwa na
hatimaye kupelekea kichwa kupasuka na ubongo kumwagika chini leo
majira ya saa tisa mchana eneo la ilala boma
Mwili
wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ukiwa
umefunikwa na kanga huku pembeni vipande vya ubongo wake vikiwa pembeni
mara baada ya kugongwa na lori na kukanyangwa kichwa na kupelekea
kichwa kupasuka na ubongo wote kumwagika chini leo majira ya saa tisa
mchana eneo la Ilala Boma. Kijana huyu anasadikiwa kuwa ni mwanafunzi
wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Msimbazi.
Askari
wa Usalama barabarani akisaidiana na baadhi ya wananchi kuubeba mwili
wa marehemu ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ili
kuupakia katika gari dogo tayari kuupeleka hospitali ya Amana.Kijana
huyu anakadiriwa kuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya
Msingi Msimbazi.
Baadhi
ya wananchi wakiutazama mwili wa marehemu ambaye amegongwa na gari na
kupelekea kupasuka kichwa na kupoteza maisha papo hapo.
Mwili
wa marehemu ukifunikwa vizuri kwaajili ya kupelekwa hospitali ya
amana.Pembeni ya mwili wa marehemu ni vipande vya ubongo mara baada ya
kukanyangwa na lori
Kijana
wa kiume ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja amepoteza
maisha mara baada ya kugongwa na lori leo majira ya Saa tisa Mchana
eneo la Ilala Boma karibia na Ofisi ya Mkuu Wa Mkoa wa Dar Es salaam.
Mara baada ya kugongwa na lori, lori hilo liliweza kukimbia na
halikujulikana ni wapi limeelekea na namba za gari hizo hazikuweza
kupatikana mara moja.
Kijana
huyu anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 14 ambaye pia shuhuda wa ajali
hii ameueleza mtandao wetu kuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi
Msimbazi Center kutokana na sare za shule alizokuwa amevaa.
Shuhuda
wa Ajali hii ambaye hakupenda jina lake kuchorwa na mtandao wetu
amesema kuwa Wakati kijana huyo anavuka barabara lori lililomgonga
lilikuwa linatokea maeneo ya buguruni na kumgonga kijana huyo. Mara
baada ya kumgonga lilimkanyaga kichwani " Lilianza tairi la mbele
kumkanyaga kichwa halafu likafuatia na tairi la nyuma ambapo
lilipelekea kichwa kupasuka vibaya na hatimaye ubongo kusambaa
barabarani kama ambavyo unao hapo chini na hatimaye lori hilo kukimbia"
alisema shuhuda huyo.
Na
hivi ndivyo shuhuda wetu alivyojibu " Kiukweli Nilishindwa kuandika
au kunakili namba ya usajili wa lori kwasababu kwanza niliposikia kitu
kizito kimegongwa na hilo lori nilijua ni mtu wa bodaboda wakati
naangalia vizuri nikaona ni kijana mdogo ndiye amegongwa na lori
likimkanyaga kichwa likiwa katika harakati ya kukimbia hapo nilishindwa
kuandika chochote kwasababu nilipigwa na butwaa na kubaki kama
bumbuwazi na mwili kushikwa na ganzi mara baada ya kuona ubongo vipande
vya ubongo chini" alisema shuhuda wetu
Mpaka
chanzo chetu kinaondoka eneo la tukio lori lililomgonga halikuweza
kupatikana wala kujulikana lilipoelekea na jina la kijana aliyepoteza
uhai papo hapo nalo halikuweza kupatikana
Chanzo: Lukaza
No comments:
Post a Comment