Watu
kumi na saba wamekufa na wengine 78 kujeruhiwa wilayani Sikonge katika
Mkoa wa Tabora baada ya basi la Sabena aina ya Scania lenye namba T570
AAM kupata ajali na kupinduka.
Basi hilo lilikuwa likitoka Tabora kwenda Mbeya.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge umbali wa kilometa 200 kusini mwa mji wa Tabora.
Miongoni wa watu waliokufa ni watoto watano, wanawake sita na wanaume sita na hadi leo mchana, miili ya watu saba ilikuwa imetambuliwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Antony Ruta, alisema basi hilo lilikuwa limejaa kupita kiasi kwani inaonekana lilikuwa na abiria zaidi ya 100.
KAMANDA WAPOLISI MKOA WA TABORA ACP ANTON RUTTA AKITOA MAELEZO KWENYE VYOMBO YA VYA HABARI KWENYE ENEO LA TUKIO
MMMOJA WA MAJERUHI WA AJALI HIYO AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI
Hata hivyo, hadi kufikia leo mchana, miili ya watu saba ilikuwa imetambuliwa na baadhi ya ndugu, ukiwemo wa askari Polisi Konstebo Kheri, wa Kituo Kikuu cha Polisi cha mjini Tabora.
Marehemu wengine waliotambuliwa ni Vitus Tulumanye, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), tawi la Tabora na Farah Inga raia wa Zimbabwe aliyekuwa akifanyakazi Tabora.
Wengine waliotambuliwa ni Ikamba Thadeo, Damalu Goma, Beatrice Kalinga ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Igoko wilayani Uyui mkoani Tabora na Madirisha ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi iliyoko wilaya Mpya ya Kaliua.
Mwalimu Madirisha anadaiwa kufuatana na watoto wanne na mkewe ambaye bado hajatambuliwa najuhudi zinaendelea za kubaini familia ya mwalimu huyo.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na aliyenusrika katika ajali hiyo kwa mwakilishi wa basi hilo mkoani Tabaro, Shaaban Mnyema, chanzo cha ajali hiyo ni lori aina ya Fuso lililokuwa limeegeshwa katika kona. Aidha Alidai kuwa kutokana na mwendo wa kasi lililokuwa nalo, dereva wa basi hilo alipojaribu kulikwepa fuso hilo ndipo 'Stearing Road' ilipokatika na kusababisha gari kuacha njia na kupinduka.
Dereva wa basi hilo Ali Nassoro, ambaye alitoroa baada ya kutoa taarifa za ajali na maelezo hayo kwa njia ya simu, alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 6.30 mchana katika eneo ambalo halina mawasiliano ya simu za mkononi.
Nassoro alisema hata katika kijiji cha Kitunda kulikuwa hakuna mawasiliano na hivyo kumlazimi kumtuma mtu kwenda Sikonge kutoa taarifa za ajali hiyo.
Baadhi ya majeruhi waliotambuliwa ni Grace Mbunga, Kayungilo Nsungu, Zena Shigela, Ndisi Ngosha, Kulwa Kija, Feni Salum, Shinje Kayogole na Emmanuel Charles.
NA KING JOFA
No comments:
Post a Comment