Emmanuel Adebayor amekamilisha mipango ya kuhamia Tottenham Hotspur kutoka Manchester City kwa kitita cha pauni milioni 5.
Mshambulizi
huyo kutoka Togo alionyesha umahiri wake msimu uliopita, akiichezea
Tottenham kwa mkopo, kwa kufunga jumla ya magoli 17 katika ligi kuu ya
Premier.
Adebayor atakuwa ni kati ya wachezaji wenye mishahara mikubwa katika klabu hiyo ya uwanja wa White Hart Lane.
Adebayor, mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akilipwa na Manchester City pauni milioni 175,000 kwa wiki.
Mshambulizi
huyo, ambaye zamani alikuwa akiichezea Arsenal, alifichua habari za
kujiunga na Tottenham kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter: “Tottenham
niko njiani! Natamani magoli. Kaeni chonjo.”
Mkataba
wa Adebayor ulikuwa uendelee kwa miaka miwili zaidi na klabu ya Man
City, na kwa kipindi kirefu katika misimu miwili iliyopita alikuwa
akiichezea Real Madrid ya Uhispania, na kisha Tottenham.
“Ninafurahi kujiunga kabisa na Spurs baada ya klabu kuelewana na Manchester City,” aliongezea Adebayor.
“Pengine
ilichukua muda mrefu kinyume na ilivyotazamiwa, lakini nimefurahi sana
kurudi Tottenham Hotspur. Nilifurahi sana nilipokuwa hapa msimu
uliopita, na ni matumaini yangu tutaweza kwa pamoja kufanikiwa hata
zaidi.”
Inafahamika kwamba Spurs walikataa kubadilisha mipango yao ya mishahara ili kufanikisha mipango ya kumpata Adebayor.
Lakini
kutokana na Adebayor kukataa kupunguziwa mshahara, mabingwa wa ligi kuu
Manchester City walikubali kuongezea zaidi tofauti ya senti
atakazopokea Adebayor katika klabu ya Tottenham, na kiwango alichozoea
Man City cha pauni 175,000.
Tottenham
watamlipa pauni 80,000 kwa wiki, na Man City ilibidi kukubali kuongezea
tofauti ya elfu 95,000 kwa wiki, ili kuyafanikisha makubaliano kati ya
vilabu hivyo viwili.
Makubaliano
hayo yanahitimisha ubishi ulioendelea kwa muda mrefu, kuhusu ikiwa
Adebayor alistahili kulipwa bakshishi na marupurupu mengineyo iwapo
angelisisitiza kuondoka Man City pasipo makubaliano kamili kati yake na
klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment