MBUNGE
wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake wameendelea kuwang’ang’ania
wadhamini wa Chama cha Wananchi (Cuf), wakiiomba Mahakama Kuu iwatie
hatiani na kuwafunga kutokana na kitendo cha kufukuzwa kwao uanachama.
Licha
ya wadhamini hao, wengine ni wajumbe wa Baraza Taifa la Uongozi la
chama hicho akiwamo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad. Januari 10, mwaka huu
Rashid na wenzake 10 waliwasilisha mahakamani hapo maombi wakitaka
iwaite wadhamani wa chama chama hicho, wajieleze sababu za kutotiwa
hatiani na kufungwa kwa kosa la kupuuza amri ya mahakama.
Maombi
hayo yalitokana na uamuzi wa Baraza la Taifa la Uongozi la chama hicho
wa Januari 4, mwaka huu kuwafukuza uanachama wa chama hicho na
kuwasimamisha wengine. Pia, katika maombi hayo wanaomba mahakama
ibatilishe uamuzi wa Baraza hilo wa kuwavua uanachama kwa madai kwamba
walikiuka Katiba ya Cuf.
Wakati
wa usikilizwaji wa maombi hayo, Hamad na wenzake katika hoja zao za
maandishi walizoziwasilisha mahakamani kupitia kwa Wakili wao, Augustine
Kusalika wanadai baraza hilo liliwafukuza uanachama wakati tayati
likiwa na amri ya mahakama kuzuia kuwafukuza.
Amri
hiyo ya mahakama ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa Januari mwaka huu
kufuatia maombi waliyoyawasilisha Januari 3, chini ya hati ya dharura.
Mwisho
No comments:
Post a Comment